Saturday, March 12, 2011

BABU WA LOLIONDO KAZUA BALAA


Magonjwa Sugu yako mengi na wagonjwa ni wengi pia. Babu Mwasapile kazi anayo mwaka huu.

Chanzo: The Citizen On Saturday 12/3/2011

Labels:

Friday, March 11, 2011

LOLIONDO KUMEZUA JAMBO


Fikra ya msanii Masoud Kipanya kuhusu yanayotokea kufuatia matibabu huko kwa BABU Loliondo

Kuna kitu ninajifunza kutokana na yanayotendelea kufuatia 'kuvumbuliwa' kwa dawa inayotibu maradhi sugu kwa mchungaji mstaafu Mwasapile. Katuni inaelezea kuwa BABU amevuta watu kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo hospitali. Najiwa na mawazo kuwa tunafarijika na kazi tunazofanya na ikiwa tunakosa kazi ya kufanya tunasononeka. Askari akikosa muhalifu haoni rana. Mwalimu akikosa mwanafunzi haoni rana. Mzibua vyoo visipoziba hajisikii. Je, inawezekana daktari asipopata mgonjwa anajisikia mambo kutokwenda sawa?

chanzo: mwananchi 10/03/2011

Labels:

ALPHA BLONDY

Mimi sio mpenzi sana wa Alpha blondy lakini inapokuja katika nyimbo zake kadhaa huwa sifichi kuonyesha huba yangu kwazo. Ijumma hii hebu tushirikiane kuutazama na kuusikiliza SWEET FANTA DIALLO.




Ijumaa njema

Labels:

Thursday, March 10, 2011

TUMAINI MPAUKO
Picha hii nimeitoa Mbeya Yetu. Katika kuwatazama mabinti hawa ambao wamechoka na kutungua na kukusanya maembe na sasa wanajiandaa kuyabeba kupelea sokoni (kama si nyumbani).




Kuna jambo nimelifikiri hapa. Sura hizi hazinionyeshi kuwa katika mabinti hawa tunatarajia madaktari, mainjinia ama wanasheria nk. Mie naona kama tayari wanaonyesha wataishia kuokota maenbe na kuyauza na kungojea kuolewa ama katika ndoa za mke/mme moja ama katika mitaala.

Labels:

Wednesday, March 09, 2011

KITOWEO HIKI MBEYA ADIMU

Mkoa wa Mbeya umekumbwa na balaa la ugonjwa kwa mnyama huyu. Kuna uwezekano mkubwa karantini ya ugugaji na usambazaji wake ikawekwa hivyo kufanya kitoweo kiwe adimu.



Hali ya mfugo si shwari.


Ni vema watumiaji wakajihadhari kwa kuhakikisha wanapata mlo wenye uthibitisho wa wahusika wa nyama hii.

Labels:

Sunday, March 06, 2011

JAMBO LIMEZUA JAMBO
Miongoni mwa hobby zangu ni kufurahia kazi za sanaa. Pengine inatokana na kusoma theory kidogo kule FPA UDSM.

Siku si nyingi story za kila pahala Tanzania na nje ya nchi kwa watanzania gumzo lilikuwa kujitokeza hadhsrani kwa 'mmiliki' wa kampuni ya Dowans. Moja ya vioja kilikuwa wahariri waliozungumza na 'mmiliki' huyo, Al-Adawi, kutoruhusiwa kumpiga picha.

Msanii Nathani Mpangala akachora katuni kuwadhihaki wahariri walioalikwa kuongea na Al-Adawi. Tazama katuni ya hii.Imetolewa hapa.



Kijasti mkorofi.

Katika usanii, Mpangala amekuja na katuni hii hapa chini kuonyesha kuchukiwa na WAHALILI kwa kuwadhihaki kwa katuni ya juu. Imetolewa hapa.



Kijasti anatafutwa

Labels: ,

Friday, March 04, 2011

Dowans wants to negotiate?

Huwa napenda sana kumsom Adama Lusekelo jinsi anavyoshambulia masuala ya kijamii kwa mtazamo mwepesi (with a light touch). Hapa anamchambua 'mmiliki' wa Dowans na uzanzibari-utanzania wake.

Adam Lusekelo


Al-Adawi mwenyewe

BY ADAM LUSEKELO
THE guy whom Tanzanians have been told owns Dowans electricity generator, Brigadier Mohamed Yahya Al Adawi, suddenly has hit town and some good investigative reporters have been doing some snooping. Just who is this guy?

Apparently Al Adawi is as Zanzibari as cloves. He was just a lowly cop in the Zanzibar constabulary under the Sultan's payroll back in 1964. He fled for his life, when the local natives were hunting for the oppressor during the bloody Zanzibar Revolution and went to his ancestral home in Oman.

Last week he came back as a businessman. "With good intentions and in the spirit of amicable resolution, it is my sincere hope that Tanesco, government and people of the United Republic of Tanzania will listen to us so that we can together see how to work to alleviate the current electricity crisis," Said Dowans owner retired Brigadier Suleiman Mohamed Yahya Al Adawi.

The Dowans chief surfaced mysteriously after Tanzanians were constantly being told that the company was owned by ghosts, represented by the MP for Igunga. Why? Because when the time was ripe the ghosts decided to give Mr Rostam the power of attorney to negotiate for them.

When did they meet? Only they know, for there is a huge age difference for them to have been childhood buddies.

In a show of goodwill, he said soon after the IOC judgment Dowans wrote to Tanzania and government seeking to engage them in discussion about available options but to date Dowans has not received any response.

Then the brig started tough talk. He has friends in international high places who could make life in Tanzania very unpleasant for us as a country that seeks to attract more foreign direct investments.

"I am deeply concerned about the future of foreign investment Tanzania would have if they seem to ignore or reject foreign direct investment," he said.

Expressing disgust at the way his company and personality have been 'wrongly depicted in the country,' and the media he insisted that Dowans was a duly registered company that was squeaky clean -- just like that. But then, he would say that, wouldn't he?

And this business of his having belonged to the sultan's coercive apparatus is not exactly comforting and raises quite a number of questions. So if he comes back three decades later in a sheep's skin, swearing that he loves Tanzania leaves eyebrows soaring.

One may wonder -- why is the brig coming now? For everyone knows that Arabia is experiencing serious turmoil. Is it a question of grabbing your loot and cutting and run? If that is the case then that is highly understandable.

You don't get rid of guys like Hosni Mubarak the pharaoh of Egypt until recently or former ruler of Tunisia, Mzee Ben Ali just like that.
adluse@gmail.co, adamlusekelo.blogspot.co.

Labels:

Thursday, March 03, 2011

VIPI BLOGU YA LUGHA

Mswahili-Msauzi Goodman alipendekeza kuanzishwa kwa blogu ya jamii ya kufundishana na kujifunza lugha mbalimbali hasa za kiAfrika. Allipendekeza hapa.




Alipendekaza kuwa blogu hii iwe ya wote tutakaopenda. Yaani tutakuwa tunaweza kuchapicha mafundisho (pengine na masahihisho ya lugha zetu). Hapa chini ni mfano wa pendekezo wa namna ya kujifunza/kufundisha lugha kwenyewe alikotoa yeye.

Swahili: "mTU", plural: "waTU"
Zulu: "umNTU", plural: "abaNTU"
Swazi: "mNTFU", plural: "baNTFU"
Kihaya: "...", plural: "...."
Kinyankole: "....", plural: "..."
Kiganda: "....", plural: "..."
Kinyambo: "....", plural: "..."

Katika somo lake hili naanza kwa kinyakyusa

Kinyakyusa: "umuNDU", plural "abaNDU"

Katika sentensi inaweza kuwa:

umuNDU uju ntali (mtu huyu mrefu)
abaNDU aba batali (watu hawa warefu)

Mafunzo mengine ameyatoa hapa kuhusu lugha za Afrika ya Kusini

Goodman anaandika "Kama wazo langu unalipenda nitumie basi email kusudi blogu hiyo nianzishe na kukutumia PASSWORDS zake kusudi wote wawili (na wengineo wapendao wazo hili) tushirikiane kuiandika. Email yangu manyanyaphiri@gmail.com"

WAZO LINA MASHIKO AMA LA?

Wednesday, March 02, 2011

PICHA HUNENA MANENO ELFU MOJA



JE, KATUNI HUNENA MANENO MANGAPI?

Labels:

HAWA The Bus Driver
Bada ya zaidi ya miaka 17 leo nimekiona tena kitabu hiki katika duka la vitabu kuukuu na nikakinunua nijikumbushe stori za dereva Hawa.



Nimekisoma kwa dakika 30 tu na kukumbuka mbali kwa kweli.Pia nimegundua nilipokisoma kwa mara ya kwanza sikukielewa vema.

Labels: