Saturday, February 27, 2010

Fikra za outing wanawake na wawanume

Eti hii ni summary ya mawazo wanayokuwa nayo wanaume (shoto) na wanawake wanapotaka/wanapotakiwa kutoka kwenda kustarehe kama vile club na kwingineko.Kuwa mwanamke kazi bwana, au?

Labels: ,

Wednesday, February 17, 2010

Remmy Ongala...!!!Leo nimefurahi kujua kuna blogu inayojishughulisha na muziki wa Tanzania. Hii intaitwa Wanamuziki Tanzania. Anayejishughulisha nayo ni mkongwe/mtaalamu John Kitime. Kwa akina siye tunaopenda muziki hasa wa zamani, ambao huwa tunafikiri dunia ya muziki ilishaisha na ujio wa bongo fleva, hapa tumefika. kuna historia, uchambuzi na ufaanuzi mkuu. hayo ya dk Remmy Ongala utayakuta huko. Asante mzee wa changamoto na mzee wa ukweli John Kitime.

Labels:

Sunday, February 14, 2010

MIAKA MI-4 YA SAUTI YA BARAGUMU
Nimekuwa kimya kwa takribani majuma mawili hivi. Nilikuwa Morogoro nikiwatumikia watu asubuhi mpaka saa moja jioni. Uchovu na kuwa mbali na mtandao vilinifanya nishindwe kublogu. Nimerejea kublogu ingawaje bado niko njiani kurudi mbeya. (Niko Dar kutoka Morogoro kwenda Mbeya - imekaaje hii??)

Nikiwa huko Moro Sauti ya Baragumu ilitimiza miaka Mi-4 toka lianzeshwe Februari 2006, New Jersey, USA. Angalia Post nilizoanza nazo wakati huo hapa. Miaka inaenda kasi mmno. Pichani ni picha niliyojipiga nikiwa hotelini Morogoro nikiwa na kashati kangu ka njano nilikokuwa nako wakati naanzisha blogu hii. nakaita kashati ka blogu.

Labels: ,