Sunday, June 27, 2010

LEO NI SHANGWE

si wanasema picha inaongea maneno 1000. Mie sisemi. Monday I am off to Dar and Moro. See you around.

Labels:

Tuesday, June 22, 2010

ADIMIKO

Nililazimika kutokuwepo hewani kwa sababu mbili. moja kuu na nyingine sio kuu kama ile kuu. Sababu kuu ni adimiko la internet (bule glali). Sababu isiyo kuu ni Kombe la Dunia. Baada ya kukosa internet ya bule sikujishughulisha kwenda mbali kuitafuta ya kulipia kwani muda ulikuwa ukigongana na mechi za WOZA 2010.

Ile napata mtandao nakumbana na habari njema ya kuenguliwa kwa refa Koman Coulibaly (pichani) aliyechezesha na kulikoroga katika mechi ya Marekani na Slovenia. 'Kama unabisha' Soma story hapa. Huyu refa alinikera sana, sio kwa sabau nawazimia marekani bali kwa kuwa ilikuwa haki yao.Nimekuwa muumini mzuri wa dini inaitwa Kombe la Dunia 2010. mpaka sasa nimelazimika kukosa mechi nne tu.

Labels: ,

Tuesday, June 08, 2010

CHEKA KIDOGONimedesa hapa

Labels:

Monday, June 07, 2010

YAMETIMIA. TAIFA STARS OUT

Taifa Stars (bluu) na wenyeji Amavubi. Picha hudubin-my-o-scope

Juzi nilitabiri uwezekano wa TAifa Stars kutolewa katika mashindano ya wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani. Sio kwamba naingilia kazi ya watabiri lakini ilijionyesha wazi tulithamini zaidi mechi ya kirafiki (kinafiki) baina yetu na Brazil kuliko mechi ya mashindano. Sikio la kufa halisikii medisini.

Labels:

Saturday, June 05, 2010

DUNIA INAPOCHEZA SOKA LA AFRIKA YA KUSINI

Kila mtu sasa anajua kombe la dunia ndio hilo araundi ze kona. hakika Duni imepigishwa kwata kucheza mpira katika mahadhi ya ki-Afrika ya Kusini. Na twende pamoja sasa...Makarapa ni vazi la kichwani kwa vichaa wa soka Afrika ya Kusini.Vuvuzela ndio Baragumu la soka huko Kunako shughuli. Hili hupagawisha wachezaji na washabiki wasioliewa. Linasubiriwa tamko baada ya mechi chache za awali kuwa liruhusiwe kuendelea ama la.


KWINGINEKO.
Mchambuzi wa soka hasa linapokuwa ni Kombe la Dunia, Madaraka Nyerere wa kijijini Butiama, anabashiri timu hizi zitaingia raundi ya Pili:

Group A - France and Mexico
Group B - Argentina and Nigeria
Group C - England and USA
Group D - Germany and Serbia
Group E - Netherlands and Cameroon
Group F - Italy and Paraguay
Group G - Brazil and Portugal
Group H - Spain and Switzerland

Anadai...

If I get a 75 of my predictions right, I will consider changing careers and move into predicting future events. Soma zaidi hapa.

Labels: , ,

'ZEMARCOPOLO' ATANGAZA NIA MOROGORO


Dk. Imani Hamza Kondo 'ZEMARCOPOLO'

Kwa wenzangu na mie tulioanza kublogu maka ya 2005/2006 na kuendelea tunamkumbuka mwanablogu mashuhuri haka kwa uchangiaji aliyekwenda kwa jina la ZEMARCOPOLO. Huyu ni Dk. Imani Hamza Kondo. Ametangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Morogoro Kusini Machariki kwa tiketi ya CCM.

Anaomba ushirikiano wa namna yoyote iwayo. Soma zaidi hapa na hapa.

Sauti ya Baragumu inamtakiwa kila la heri.

Labels:

SWALI - USAFIRI DAR ES SALAAM
Kuna mwananchi mwenye nia njema anauliza uwezekano wa kutumia reli kupunguza kero ya usafiri dar es salam.


Reli ikikarabatiwa

Anauliza...

Naamini hamjambo Waungwana.

Nina kaswali kamoja kadogo hapa, ambako kananizingua labda kutokana na upeo wangu mdogo au uzee! Hivi ni kwanini hakuna usafiri wa TRENI katika jiji la dar es Salaam wakati miundombinu ipo?

Kuna Reli toka Pugu hadi Stesheni, Ubungo Maziwa hadi Stesheni, Keko hadi Stesheni, Mivinjeni hadi stesheni. hapa mahali hapahitaji mabehewe ya lakshari, hayo yaliyolala kule yadi Ilala, yanafaa. hatuhitaji vichwa vikubwa, hata vile vya shantingi vinafaa!

Msaada jamani mwenzenu nachanganyikiwa!!

ABU MSEMO

Nimeitowa kwa Lady JayDee

Labels:

MIE NAONA KAMA TUSHAFUNGWA NA RWANDA VILE
Taifa Stars

Karibu juma zima lililopita stori za kisoka zimetawaliwa na ujio wa timu ya soka ya taifa la Brazil kucheza na katimu ketu Taifa Stars. Mengi yamezungumzwa kuanzia urari wa kuileta Brazil na hali halisi ya uchumi wetu na matatizo yetu. Hili halinihusu sana kwani ningelikuwa mimi ningeliamua vinginevyo.

Kabla ya mechi na Brazil keshokutwa, Taifa Stars watakuwa na kibarua cha kujaribu kufuzu kucheza fainali za wachezaji wachezao ligi za nyumbani yaani CHAN. Jumapili watakuwa ugenini Kigali kujaribu kuwafunga wenyeji AMAVUBI ili wafuzu. Lakini mie naona kama tushafungwa mechi hii kwa sababu kila kona watu wameipa kipaumbele mechi ya 'kishkaji' na Brazil kuliko mechi ya mashindano na Rwanda. Sijamsikia mtu akipanga mikakati ya kuwafunga Rwanda. Naisikia mikakati ya kulipa kiingilio cha malaki kuwaona wachezaji wa Brazili wakibadilishana jasho na wa kwetu. Nadhani hata wachezaji wa Stars wanasubiria mechi ya Brazil zaidi kuliko ya Rwandwa. Yangu macho lakini nawapa Rwanda 80% kufuzu

Labels: