Friday, February 25, 2011

MAPENZI YA TAJIRI NA MASIKINI

Yanaweza kuwapo? au ni Kizungumkuti. Kwa ijumaa hii tulitafakari hili kwa kumsikiliza Vumilia katika songi lake hili Tatizo UmasikiniIjumaa Njema

Wednesday, February 23, 2011

DOWANS KAPIGWA PICHA !!!
Mmiliki wa kampuni inayosemwa kutaka kuidhoofisha mifuko ya watanzania, Brig. Jenerali Sulaiman Mohamed yahya Al-Adawi aliripotiwa kukataa kupigwa picha.
Jana majamaa yamemtwanga picha akikagua "asset"zake.

HIVI KWA NINI AJIFICHE?

Labels:

Tuesday, February 22, 2011

MAKUBALIANO KIKAO CHA WANA-MALANGALI
Makubaliano haya sio rasmi. Nimetumiwa na mtu aliyekuwako katika kikao kilichofanyika 5/2/2011.Baadhi ya wasomaji wa blogu hii walitaka kujua yaliyojiri huko.Wanafunzi Malangali.

Yafuatayo ni makubaliaono

Hakika kikao kilikuwa kizuri sana, kulikuwa na umati wa 'Wanamalangali' kama 40 hivi. Kamati ya muda ya kuratibu mkutano huo iliteuliwa, ikiongozwa na Stan Nyavanga na wenzake. Walianza kwa kukumbushana mazingira ya sasa ya shule na kuangalia mahitaji ya sasa ya shule yetu.

Makubaliano:
1. Kuunda kamati rasmi ya kutathmini changamoto zinazoikabili shule kwa sasa na kuangalia namna ya kukabili changamoto hizo (ikiwemo kushuka kitaaluma katika maka ya hivi karibuni)

2. Kuunganisha wanafunzi wote waliosoma Malangali kwa njia ya mtandao na njia ya ana kwa ana (ili kuwapa fursa hata wale walio mbali na Malangali) kupata taarifa za mara kwa mara na kuchangia maendeleo ya shule.

3. Kuitisha mkutano mwingine mapema iwezekanavyo ili kuanzisha 'Alumni' ambayo itakuwa na katiba rasmi na uongozi rasmi kwa ajili ya kushughulikia changamoto za shule.

4. Kuwakutanisha wana Malangali angalau mara moja kwa mwaka

5. Kuanza kuchangia ununuzi wa vitabu vya kiada na ziada na kuvikabidhi shuleni kwa utaratibu utakaopangwa, ili kukuza taaluma. Lengo ni kuongeza vitabu ambavyo tumesaidia kuvichakaza kwa elimu tuliyonayo ili wadogo zetu nao waweze kusoma.

Maazimio hayo yatajadiliwa zaidi katika kikao kijacho.

Mwalyoyo

Labels:

Thursday, February 17, 2011

SAFARINI MATAMBA
Jana siku Kuu ya Maulid mimi na waminifu wangu tuliona tukaisherehekee kijiji cha Matamba wilayani Makete. Sio mbali sana na Mbeya Mjini. Ukiwa unaelekea Iringa unachepukia Chimala kuelekea milimani. Ni Milima iliyo mikali huwezi kudhani kuna hata barabara hukoHapa ni katikati ya safari yetu. Chini kule chini ndio mji wa Chimala. Hatuko kwenye ndege ama helikopta. Kwa mbali unaweza kuona barabara iendayo katika mashamba ya mpunga ya usangu. Pia unaweza kuona mashamba ya mpunga.


Ukifika Matamba shurti upozee koo. Ulanzi huo. So sweeet.
Ukiwa Matamba unakuwa karibu kabisa na vivutio vya kitalii kama ziwa Ngozi na Hifadhi ya taifa ya Kitulo. Huko tutafika siku zingineSafari ya kurudi. Chimala kuleeeeeee mbali.em>


Waaminifu wangu (shoto na kati)na dereva wetu (kulia).

Labels:

Monday, February 14, 2011

GUARDIAN ANGELKule Swahili Time nikutana na habari ya Kitabu hiki. Kimeandikwa na mganda mmoja kuhusu viongozi wa zamani wa Afrika Mashariki kama Idd Amin, Julius Nyerere, Milton Obote na wengine. Kinachambuliwa kuwa kinatoa wasifu wa hawa watu kwa sura nyingine ambayo wengi hatuijui. Stori zaidi soma hapa.

Nauliza upatikanaji wake. Kuna mtu anaweza kukileta Tanzania?

Labels:

Monday, February 07, 2011

KATUNI ZETU NA YANAYOTOKEA NCHI ZA KIARABU


Kitanzi cha udhalimu, udikteta na ung'anga'nizi wa madaraka hola!!!!

Credit:The Citizen,on Sunday 30/Jan/2011

Labels:

Friday, February 04, 2011

MIAKA 5 YA SAUTI YA BARAGUMU


Blogger John Mwaipopo ndani ya mablogu

Juzi blogu hii ilitimiza miaka mitano hewani. nilitamani sana kujipongeza lakini siku wa na internet. Milima na mabonde nimeivuka na sasa Sauti ya Baragumu imefikisha miaka mitano. Nilianza tarehe 2 Feb. 2006 na post hizi hapa. Naam kublog ni addiction ambayo inakutanisha watu. Na nitaendelea panapo majaliwa.

Labels: