Thursday, July 31, 2008

UDSM

Ukuta huu ni wa makataba kuu ya UDSM. Matangazo ya kila namna utayakuta yamebandikwa na mengie kubanduliwa namna hii. Hivi haya ni matumizi sahii ya ukuta tena wa chuo kikuu? Haman namna mbadala ya kubandika matangazo?


Nilipokuwa mwanafunzi mwaka 2001 tulipewa assignment ya kikundi kutoa tafsiri sahihi au inayokaribiana na muonekano wa sanamu hii iliyopo Chuo Kikuu Mlimani, mbele ya makataba kuu. Kila mtu akasema lake. Sijui wengine wanasemaje?

Labels: