Friday, March 11, 2011

LOLIONDO KUMEZUA JAMBO


Fikra ya msanii Masoud Kipanya kuhusu yanayotokea kufuatia matibabu huko kwa BABU Loliondo

Kuna kitu ninajifunza kutokana na yanayotendelea kufuatia 'kuvumbuliwa' kwa dawa inayotibu maradhi sugu kwa mchungaji mstaafu Mwasapile. Katuni inaelezea kuwa BABU amevuta watu kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo hospitali. Najiwa na mawazo kuwa tunafarijika na kazi tunazofanya na ikiwa tunakosa kazi ya kufanya tunasononeka. Askari akikosa muhalifu haoni rana. Mwalimu akikosa mwanafunzi haoni rana. Mzibua vyoo visipoziba hajisikii. Je, inawezekana daktari asipopata mgonjwa anajisikia mambo kutokwenda sawa?

chanzo: mwananchi 10/03/2011

Labels:

7 Comments:

At 7:40 AM, Blogger Simon Kitururu said...

Madaktari hata wakiwa na wagonjwa si nasikia sikuhizi dili ni Ubunge?

 
At 7:54 AM, Blogger John Mwaipopo said...

nani hapendi kusinzia .... sorry 'kuombea taifa' (kama alivyofanya mheshimiwa nanihii) kule mjengoni dodoma?

kwa msiojua, kuna aina mpya ya kuliombea taifa ukiwa bungeni. ichunguzeni.

 
At 7:58 AM, Blogger John Mwaipopo said...

nani hapendi kusinzia .... sorry 'kuombea taifa' (kama alivyofanya mheshimiwa nanihii) kule mjengoni dodoma?

kwa msiojua, kuna aina mpya ya kuliombea taifa ukiwa bungeni. ichunguzeni.

 
At 8:02 AM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Mimi napenda kuwa kinyuma sidhani kama una kazi na ukikosa cha kufanya kama ni raha. Basi naona wote tutagombe huo Ubunge

 
At 9:23 AM, Blogger chib said...

Ni wakati muafaka wa madokta na wauguzi kuchukua likizo :-)

 
At 10:56 AM, Blogger malkiory said...

Habari zinadai kuwa mkuu wa kaya pamoja na mpinzani wake wa karibu katika uchaguzi mkuu uliopita walikuwa miongoni mwa wa watu waliokunywa chai ya Babu, hahahaaha.

 
At 11:00 AM, Blogger John Mwaipopo said...

mkuu Matiya kama ndio hivyo si vema kuwazuia watu kuendelea kumiminika kwa BABU. kulikuwa na nia ya kutaka kumshurutisha babu kuacha kutoa TEMBE zake. sijui kama wamefanikiwa kuzui utoaji tiba. Babu ameifunika hata CHADEMA!

pili kuwa kuna tetesi kuwa watu wadogo kwa wakubwa wamekwenda kunywa 'chai' inadhihirisha ni jinsi gani waTZ weng tunatembea tukiwa na maradhi tele miilini mwetu.

 

Post a Comment

<< Home