Sunday, March 06, 2011

JAMBO LIMEZUA JAMBO
Miongoni mwa hobby zangu ni kufurahia kazi za sanaa. Pengine inatokana na kusoma theory kidogo kule FPA UDSM.

Siku si nyingi story za kila pahala Tanzania na nje ya nchi kwa watanzania gumzo lilikuwa kujitokeza hadhsrani kwa 'mmiliki' wa kampuni ya Dowans. Moja ya vioja kilikuwa wahariri waliozungumza na 'mmiliki' huyo, Al-Adawi, kutoruhusiwa kumpiga picha.

Msanii Nathani Mpangala akachora katuni kuwadhihaki wahariri walioalikwa kuongea na Al-Adawi. Tazama katuni ya hii.Imetolewa hapa.



Kijasti mkorofi.

Katika usanii, Mpangala amekuja na katuni hii hapa chini kuonyesha kuchukiwa na WAHALILI kwa kuwadhihaki kwa katuni ya juu. Imetolewa hapa.



Kijasti anatafutwa

Labels: ,

7 Comments:

At 7:43 AM, Blogger Fadhy Mtanga said...

ha ha ha ha haaaaaaaa Nathan Mpangala ni mmoja wa wachora katuni niwapendao toka miaka na miaka.

safi sana bro

 
At 1:24 AM, Blogger emuthree said...

Duuh, kweli katuni inaweza ikatoa meseji ukabaki umeduwaa. hongera Mpangala, na hongera mkuu kwa kutuwekea hii hewani!

 
At 4:50 AM, Blogger Fita Lutonja said...

kweli katuni ni zaidi ya maneno au maadishi kwani inaweza kuelezea maana zaidi ya elfu moja na zaidi. Asante sana

 
At 12:06 PM, Blogger Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kuna watu wanasema kwamba hili lililotokea kwa huyu mmiliki wa Dowans wa kuwapiga mkwara wa kutopigwa picha na waandishi wa habari na kweli ikawa hivyo haiwezekani kwa wakati huu ambapo kuna kamera za siri, kwenye simu na mapaparazi kila kona.

Inashangaza na kuibua maswali mengi kuhusu dhima na utaalamu wa waandishi wetu hawa. Na Mpangala kawapatia kabisa !

 
At 11:35 PM, Blogger John Mwaipopo said...

swali ulilojiuliza profesa matondo limesumbua akili za walio wengi kwa kweli. ni kama vile walikubaliana tu kuwa 'hatukupigi picha mzee'.

ila mwandishi-mpigapicha mashuhuri muhidin issa michuzi amekiti kutoalikwa kwenye 'hafla' ile. anadai kama angelialikwa basi mvua inyeshe jua liwake angelipata taswira.

 
At 1:01 AM, Blogger emuthree said...

Lakini kiustaraabu kama mumealikwa mkaambiwa `hakuna kupiga picha' kweli mtajiiba mpige picha..hiyo nazungumzia `kiustraabu' au kiheshima.
Ila jamaa kwanini alikataa kupigwa picha, kama alikuwa katenda haki?

 
At 7:16 PM, Blogger Mbele said...

Katuni ni bomba. Safi sana.

Kuhusu suala la kumpiga picha Dowans wakati yeye alikataa, naona utata mwingi.

Naamini kuwa mtu ana haki ya kukubali au kukataa kupigwa picha. Huwa nawafundisha wanafunzi mbinu na maadili ya utafiti unaohusu wanadamu, na hapo msisitizo mojawapo ni hatuna ruhusa ya kumrekodi mtu au kumpiga picha bila ridhaa yake.

Kwa msingi huu, Dowans alikuwa na haki ya kusema asipigwe picha, na waandishi walitakiwa kufuata matakwa yake.

Ni sawa na tunavyopaswa kuheshimu haki ya watu mitaani. Hatupaswi kuwapiga picha bila ridhaa yao.

Lakini utata unakuja tukizingatia kuwa hii ya Dowans ilikuwa ni shughuli ya kuongea na vyombo vya habari. Shughuli hii hujumlisha vinasa sauti, kamera, na kadhalika. Sasa kwa Dowans kuitisha mkutano na vyombo vya habari halafu aseme asipigwe picha ni kitendawili ambacho naona taabu kukitatua.

 

Post a Comment

<< Home