Thursday, March 03, 2011

VIPI BLOGU YA LUGHA

Mswahili-Msauzi Goodman alipendekeza kuanzishwa kwa blogu ya jamii ya kufundishana na kujifunza lugha mbalimbali hasa za kiAfrika. Allipendekeza hapa.
Alipendekaza kuwa blogu hii iwe ya wote tutakaopenda. Yaani tutakuwa tunaweza kuchapicha mafundisho (pengine na masahihisho ya lugha zetu). Hapa chini ni mfano wa pendekezo wa namna ya kujifunza/kufundisha lugha kwenyewe alikotoa yeye.

Swahili: "mTU", plural: "waTU"
Zulu: "umNTU", plural: "abaNTU"
Swazi: "mNTFU", plural: "baNTFU"
Kihaya: "...", plural: "...."
Kinyankole: "....", plural: "..."
Kiganda: "....", plural: "..."
Kinyambo: "....", plural: "..."

Katika somo lake hili naanza kwa kinyakyusa

Kinyakyusa: "umuNDU", plural "abaNDU"

Katika sentensi inaweza kuwa:

umuNDU uju ntali (mtu huyu mrefu)
abaNDU aba batali (watu hawa warefu)

Mafunzo mengine ameyatoa hapa kuhusu lugha za Afrika ya Kusini

Goodman anaandika "Kama wazo langu unalipenda nitumie basi email kusudi blogu hiyo nianzishe na kukutumia PASSWORDS zake kusudi wote wawili (na wengineo wapendao wazo hili) tushirikiane kuiandika. Email yangu manyanyaphiri@gmail.com"

WAZO LINA MASHIKO AMA LA?

3 Comments:

At 7:51 AM, Blogger Fadhy Mtanga said...

mie nichangie katika lugha ya kibena....

singular....'munu' plural...'vanu'

kwa mfano wako.

mtu huyu mrefu

'munu uyu mtali'

watu hawa warefu

'vana ava vatali'

nitafurahi nami kushiriki katika blog hiyo

 
At 7:52 AM, Blogger Fadhy Mtanga said...

hapo chini ni vanu na siyo vana. ukisema vana ni plural ya 'watoto' ambayo singular yake ni 'mwana'

ni makosa wakati nikichapa.

 
At 8:21 AM, Blogger John Mwaipopo said...

miaka ile bado hata kuanza shule niliwahi kuishi sehemu panaitwa ulembwe huko njombe. lugha zangu zilikuwa kiswahili na kibena. nilikujua kibena barabara kwa sababu ya uwepesi wa utoto katika kujifunza lugha. kwa hiyo, hapo fadhy ulipokuwa na kwikwi ya typingi nilishakuelewa longi.

kuhusu kujumuika katika blogu hii, unachotakiwa kufanya ni kumuandikia ndugu goodman moja kwa moja kwa e-mail yake. nadhani yuko katika mchakato wa mwisho-mwisho

 

Post a Comment

<< Home