LOLIONDO KUMEZUA JAMBO
Fikra ya msanii Masoud Kipanya kuhusu yanayotokea kufuatia matibabu huko kwa BABU Loliondo
Kuna kitu ninajifunza kutokana na yanayotendelea kufuatia 'kuvumbuliwa' kwa dawa inayotibu maradhi sugu kwa mchungaji mstaafu Mwasapile. Katuni inaelezea kuwa BABU amevuta watu kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo hospitali. Najiwa na mawazo kuwa tunafarijika na kazi tunazofanya na ikiwa tunakosa kazi ya kufanya tunasononeka. Askari akikosa muhalifu haoni rana. Mwalimu akikosa mwanafunzi haoni rana. Mzibua vyoo visipoziba hajisikii. Je, inawezekana daktari asipopata mgonjwa anajisikia mambo kutokwenda sawa?
chanzo: mwananchi 10/03/2011
Labels: ambilikile mwasapile

