Thursday, May 02, 2013

Mei Mosi 2013 Hapa nipo na wafanyakzi wenzangu katika maandamano ya Mei Mosi. Maandamano yalipokelewa na Rais JK. Jambo kuu lililonifurahisha juu ya ujio wa rais mkoani Mbeya, pamoja na shughuli nzima ya Mei Mosi, ni ukarabari wa barabara. Barabara ulikopitishwa msafara wa rais zilifukiwa mashimo yote. Mimi hutumia barabara ya Karume (Mafiati-Mjini) karibu kila siku. Mashimo yote yamefukiwa. Sasa sijajua wahusika hawakuyaona kabla ya sherehe hizi au ni mgeni njoo mwenyeji apone. Karibu tena Mei Mosi, Karibu tena rais.