Wednesday, March 09, 2011

KITOWEO HIKI MBEYA ADIMU

Mkoa wa Mbeya umekumbwa na balaa la ugonjwa kwa mnyama huyu. Kuna uwezekano mkubwa karantini ya ugugaji na usambazaji wake ikawekwa hivyo kufanya kitoweo kiwe adimu.



Hali ya mfugo si shwari.


Ni vema watumiaji wakajihadhari kwa kuhakikisha wanapata mlo wenye uthibitisho wa wahusika wa nyama hii.

Labels:

5 Comments:

At 1:03 AM, Blogger emuthree said...

Mnyama huyo wengine wanamuita `kiti moto' wengine `chakula cha bwana' wengine ...nguruwe...wengine `shwaini' ilimradi ana majina kadha wa kadha...mimi kwakweli naona asingeliwa kwasababu ana mafuta mengi sana....sasa ndio hayo magonjwa, achia yale yanayojificha kwa ajili ya mafuta mengi!

 
At 3:25 AM, Blogger Upepo Mwanana said...

Pole kwa wale wanakimiso!

 
At 4:12 AM, Blogger Simon Kitururu said...

Mdudu anaugulia mdudu gani tena huko?

Maana hujatutajia mgonjwa wetu anaumwa nini katika dondoo!:

 
At 4:15 AM, Blogger John Mwaipopo said...

ngoja nimpigie mfugani mmoja simu lakini nasikia ni kama (au ni yenyewe)ile ilitokea Mexico. MAFUA YA NGURUWE. kitu kama hicho.

 
At 4:21 AM, Blogger Goodman Manyanya Phiri said...

Sisi hatuli kabisa!

Kisa na mkasa: anapochinjwa (wengine humpiga na nyundo kwanza) analiaga "Phiiiirrrriiii! Phirrrriii! Nisaidieeee!!!"

Sasa wewe utawezaje, kama huna roho ngumu, kumla jamaa naye alikufa nakukutia huzuni kwa kuomba msaada kwako umwokoe?

 

Post a Comment

<< Home