Saturday, May 28, 2011

UCHOKOZI...!!"ACHA NINYWE KWA RAHA ZANGU MAANA NIMESHAUA ILE SHEITWAN USAMA! HAHAAAAAAAAAAAAAAAA" (Nukuu imetoka hapa)

Labels:

Monday, May 23, 2011

KICHWA CHA HABARI

Huku ku-balansi vichwa vya habari magazetini sasa balaa.
Majira Ijumaa Mei 20

Labels:

Friday, May 20, 2011

NGUVU YA MABLOGUpichani mamblogu yalivyokuwa yakionekana leo

Mablogu mengi leo yalilipoti kifo cha mnajimu huyu. Pengine ni kwa umaarufu wake aliojijengea tanzania kwa zaidi ya miaka 40, umaarufu ambao hivi karibuni kuna watu walianza kuutia shaka.

Mungu aiweke roho ya marehemu/hayati mahali anapostahili

Ninachojifunza hapa kuhuhu kublogu ni kuwa kumbe mablogu yanaweza kupeleka ujumbe fulani kwa haraka na kufaniniksha jambo fulani. au?

Labels:

Wednesday, May 11, 2011

YA KALE DHAHABUJamaa fulani yuko na jamaa yake Frank Mwasyeba baada ya mtihani mmoja wa taifa wa Kidato cha nne. Mwaka ni 1996. Nani anaweza kubashiri ni shule gani hii?

Labels:

Tuesday, May 10, 2011

HONGERA DA'MIJA KUBLOGU MIAKA SITA

Nimepekenyua blogu zetu za Kiswahili (Tanzania) na kugundua blogu ya Da'Mija Shija Sayi (pichani) imetimiza miaka sita juzi tarehe 8. Huyu mdada ni miongoni mwa ma-bloga wa kitanzania wa kwanza kabisa(Pengine zile 10 za kwanza yumo. pengine).
Da'Mija mwenyewe enzi hizo

Blogu yake ni kongwe kuliko hata ya Michuzi na nyingine nyingi. Huu hasa ndio wakati huwa nauita kwa kimombo 'when blogs were really blogs'. Hapa chini ni sehemu ya hodi yake


"Ngo...ngo..ngo... hodiii, jamani wenyewe mpoo?...inaelekea wametoka, ngoja niache ujumbe mlangoni.

Wanablogu,
Nilipita kwenu lakini inaelekea hamkuwepo, nia hasa ilikuwa nikuwapa taarifa kwamba nami nimeingia katika ulimwengu wa blogu..."HONGERA MWANAKWETU

Labels: