TUMAINI MPAUKO
Picha hii nimeitoa Mbeya Yetu. Katika kuwatazama mabinti hawa ambao wamechoka na kutungua na kukusanya maembe na sasa wanajiandaa kuyabeba kupelea sokoni (kama si nyumbani).
Kuna jambo nimelifikiri hapa. Sura hizi hazinionyeshi kuwa katika mabinti hawa tunatarajia madaktari, mainjinia ama wanasheria nk. Mie naona kama tayari wanaonyesha wataishia kuokota maenbe na kuyauza na kungojea kuolewa ama katika ndoa za mke/mme moja ama katika mitaala.
Labels: matumaini hafifu
5 Comments:
Hafifu, ndiyo!
lakini yamo (kama samaki wadogo katika bahari yao papa)
Mwanzo mgumu usikate tamaa kaka John tutafika tu! Ila duh, nimezitamani hizo EMBE:-(
Akina Rais Nyerere walitokea hukuhuku!
simon kama sijasahau sana hayati nyerere pamoja na kutokea katika mazingira kama haya pia alikuwa mtoto wa chifu hivi, kitu kilichopeleka kupata upendeleo wa watoto wa machifu kupelekwa shuleni. angelikuwa anatokea 'huku kwetu' sina uhakika sana kama angeli....
@John: Ni kweli usemalo!:-(
Post a Comment
<< Home