SWALI - USAFIRI DAR ES SALAAM
Kuna mwananchi mwenye nia njema anauliza uwezekano wa kutumia reli kupunguza kero ya usafiri dar es salam.

Reli ikikarabatiwa
Anauliza...
Naamini hamjambo Waungwana.
Nina kaswali kamoja kadogo hapa, ambako kananizingua labda kutokana na upeo wangu mdogo au uzee! Hivi ni kwanini hakuna usafiri wa TRENI katika jiji la dar es Salaam wakati miundombinu ipo?
Kuna Reli toka Pugu hadi Stesheni, Ubungo Maziwa hadi Stesheni, Keko hadi Stesheni, Mivinjeni hadi stesheni. hapa mahali hapahitaji mabehewe ya lakshari, hayo yaliyolala kule yadi Ilala, yanafaa. hatuhitaji vichwa vikubwa, hata vile vya shantingi vinafaa!
Msaada jamani mwenzenu nachanganyikiwa!!
ABU MSEMO
Nimeitowa kwa Lady JayDee
Labels: usafiri dar es salaam

