Saturday, June 05, 2010

SWALI - USAFIRI DAR ES SALAAM
Kuna mwananchi mwenye nia njema anauliza uwezekano wa kutumia reli kupunguza kero ya usafiri dar es salam.


Reli ikikarabatiwa

Anauliza...

Naamini hamjambo Waungwana.

Nina kaswali kamoja kadogo hapa, ambako kananizingua labda kutokana na upeo wangu mdogo au uzee! Hivi ni kwanini hakuna usafiri wa TRENI katika jiji la dar es Salaam wakati miundombinu ipo?

Kuna Reli toka Pugu hadi Stesheni, Ubungo Maziwa hadi Stesheni, Keko hadi Stesheni, Mivinjeni hadi stesheni. hapa mahali hapahitaji mabehewe ya lakshari, hayo yaliyolala kule yadi Ilala, yanafaa. hatuhitaji vichwa vikubwa, hata vile vya shantingi vinafaa!

Msaada jamani mwenzenu nachanganyikiwa!!

ABU MSEMO

Nimeitowa kwa Lady JayDee

Labels:

2 Comments:

At 3:57 AM, Blogger Fadhy Mtanga said...

Mi naunga mkono hoja hiyo. Ingetatua kwa kiasi kikubwa sana tatizo la usafiri jijini.

 
At 4:42 AM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Yaani ni kweli kabisa ingepunguza hayo mafoleni ya hizo daladala kabisa na kila mtu angeakuwa anasafiri kwa raha mustarehe kabisa.

 

Post a Comment

<< Home