Tuesday, June 22, 2010

ADIMIKO

Nililazimika kutokuwepo hewani kwa sababu mbili. moja kuu na nyingine sio kuu kama ile kuu. Sababu kuu ni adimiko la internet (bule glali). Sababu isiyo kuu ni Kombe la Dunia. Baada ya kukosa internet ya bule sikujishughulisha kwenda mbali kuitafuta ya kulipia kwani muda ulikuwa ukigongana na mechi za WOZA 2010.

Ile napata mtandao nakumbana na habari njema ya kuenguliwa kwa refa Koman Coulibaly (pichani) aliyechezesha na kulikoroga katika mechi ya Marekani na Slovenia. 'Kama unabisha' Soma story hapa. Huyu refa alinikera sana, sio kwa sabau nawazimia marekani bali kwa kuwa ilikuwa haki yao.



Nimekuwa muumini mzuri wa dini inaitwa Kombe la Dunia 2010. mpaka sasa nimelazimika kukosa mechi nne tu.

Labels: ,

3 Comments:

At 4:39 AM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Duh! kazi kwelikweli nne tu?

 
At 9:57 AM, Blogger Fadhy Mtanga said...

kaka pole sana kwa adimiko hilo. nami nimekuwa mwumini mzuri mno kwani hadi sasa sijakosa mechi hata moja. umeme ulipokatika radio one ikanitoa kimasomaso. ila nina majonzi kwa timu za Afrika.

 
At 10:13 AM, Blogger chib said...

Blogu zimepungua sana soko. Mie ni muumini mzuri sana wa kombe la dunia, cha ajabu kazi zimekuwa nyingi sana kwa sasa, kiasi kwamba nimelazimika kukosa kuona baadhi ya mechi

 

Post a Comment

<< Home