Wednesday, April 13, 2011

NITAREJEA
Nimeadimika mtandaoni kutokana na kuwa 'bize' na mambo fulani. Pia niko safarini morogoro na dar es salaam. sipati muda sana wa kuwa na internet.


Panapo majaliwa nitarejea hewani.

Labels:

Monday, July 19, 2010

NIMEWAHI KUWA PWEZA

Awali ya yote nikusalimieni wote ambao mlikuja hapa lakini mkanikosa. Sababu za kutopatikana zilikuwa mbili. Mosi nilikuwa safarini ambako kulinibana hata kushindwa kupata internet. Hata nilipopata wasaa wa kuchungulia internet, sababu ya pili, mtandao haukuwepo.

Wakati wa mimi kutokuwepo hewani kombe la dunia liliendelea na kumalizika. Katika matukio yaliyonisikitisha kuhusu kombe la dunia la mwaka huu ni kutolewa 'timu yangu ya Brazil' katika hatua ya pili tu. Huwa nawapenda sana Brazil.



Flagi la Brazil

Kabla ya Kombe la Dunia kuanza nilitoa angalizo na kukata tamaa kwangu kuhusu kufanya vema Brazil. Baada ya kusikia Brazil wanakuja kucheza na Taifa Stars niliogopa na kuandika sehemu fulani maneno haya chini.Kamba unabisha soma hapa, nenda maoni ya 11

kwa nia njema tu nawaomba brazil wasije kucheza na taifa stars. stars sio kipimo cha brazil. labda ni kipimio cha kupunguza ukali wa brazil.

pili stars imekuwa ikizipa nuksi timu zinazocheza nazo kwa maandalizi ya mashindano makubwa. walianza new zealand. walipoenda afrika kusini kwenye kombe la shirikisho wakawa urojo na kutolewa mapema.

wakafuata ivory coast. walipenda angola kwenye AFCON wakawa asusa, wakatolewa mapemaa.

sasa brazil ndio wanataka kuja kupata upako wa kufanya vibaya.

kwa mashindano ya world cup mwaka huu hali ya hewa ya dar es salaam haifai kwa training. Dar ni joto, Durban ni baridi. labda brazil waende njombe.


Baada ya Brazili kutolewa nikasikitika lakini nikawa nimetabiri kama pweza paulo alivyokuwa akitabiri vyema.

Labels: ,

Tuesday, June 22, 2010

ADIMIKO

Nililazimika kutokuwepo hewani kwa sababu mbili. moja kuu na nyingine sio kuu kama ile kuu. Sababu kuu ni adimiko la internet (bule glali). Sababu isiyo kuu ni Kombe la Dunia. Baada ya kukosa internet ya bule sikujishughulisha kwenda mbali kuitafuta ya kulipia kwani muda ulikuwa ukigongana na mechi za WOZA 2010.

Ile napata mtandao nakumbana na habari njema ya kuenguliwa kwa refa Koman Coulibaly (pichani) aliyechezesha na kulikoroga katika mechi ya Marekani na Slovenia. 'Kama unabisha' Soma story hapa. Huyu refa alinikera sana, sio kwa sabau nawazimia marekani bali kwa kuwa ilikuwa haki yao.



Nimekuwa muumini mzuri wa dini inaitwa Kombe la Dunia 2010. mpaka sasa nimelazimika kukosa mechi nne tu.

Labels: ,