Saturday, June 05, 2010

DUNIA INAPOCHEZA SOKA LA AFRIKA YA KUSINI

Kila mtu sasa anajua kombe la dunia ndio hilo araundi ze kona. hakika Duni imepigishwa kwata kucheza mpira katika mahadhi ya ki-Afrika ya Kusini. Na twende pamoja sasa...



Makarapa ni vazi la kichwani kwa vichaa wa soka Afrika ya Kusini.



Vuvuzela ndio Baragumu la soka huko Kunako shughuli. Hili hupagawisha wachezaji na washabiki wasioliewa. Linasubiriwa tamko baada ya mechi chache za awali kuwa liruhusiwe kuendelea ama la.


KWINGINEKO.
Mchambuzi wa soka hasa linapokuwa ni Kombe la Dunia, Madaraka Nyerere wa kijijini Butiama, anabashiri timu hizi zitaingia raundi ya Pili:

Group A - France and Mexico
Group B - Argentina and Nigeria
Group C - England and USA
Group D - Germany and Serbia
Group E - Netherlands and Cameroon
Group F - Italy and Paraguay
Group G - Brazil and Portugal
Group H - Spain and Switzerland

Anadai...

If I get a 75 of my predictions right, I will consider changing careers and move into predicting future events. Soma zaidi hapa.

Labels: , ,

Thursday, May 13, 2010

Nani Huyu?



'a healthy mind dwells in a healthy body'
Sasa ile ligi inayotupa kichaa ya Uingereza imekwisha, tena vizuri, basi sasa raha ni kujipa wenyewe. Way back in his final year UDSM 2002. Mhh! anataka kurejea enzi zake sijui ataweza? ijumaa njema.

Labels: ,

Wednesday, May 12, 2010

MSAADA TUTANI


Wababe wa Ligi Kuu ya Uingereza wakijinafasi na kombe lao

Ikiwa ni juma la kusherehekea ushindi wa Chelsea wa Ligi Kuu ya Uingereza (najua huu sio wimbo mzuri kwa Chib na Fadhy Mtanga)naomba kuuliza swali. Jumapili ile 'tukufu ya mapinduzi' ilitazamiwa washindi ama wawe Chelsea (99%)ama Manchester United (1%)ilikuwaje kombe lenyewe likawepo Stanford Bridge? Ingekuwaje kama ingetokea miujiza Manchester akabahatisha? Au kulikuwa na makombe mawili? Na kama ni hivyo, huwa inakuwaje ikiwa timu zaidi ya 2 (sema 4 za miji tofauti) zinatazamiwa kunyakua ubingwa? Kombe lilikuwa wapi kabla ya dakika ya mwisho?

Ninaamini katika ufanisi wa usafiri uingereza hasa wa treni na anga lakini kati ya London (waliko Chelsea)na Manchester ni zaidi ya Kilomita 263. Je kombe lilisafirishwa katika dakika chache baada ya mipira kumalizika kote. Natamani kujua nini kilitokea ama nini hutokea.

Labels: , ,