Saturday, June 05, 2010

MIE NAONA KAMA TUSHAFUNGWA NA RWANDA VILE
Taifa Stars

Karibu juma zima lililopita stori za kisoka zimetawaliwa na ujio wa timu ya soka ya taifa la Brazil kucheza na katimu ketu Taifa Stars. Mengi yamezungumzwa kuanzia urari wa kuileta Brazil na hali halisi ya uchumi wetu na matatizo yetu. Hili halinihusu sana kwani ningelikuwa mimi ningeliamua vinginevyo.

Kabla ya mechi na Brazil keshokutwa, Taifa Stars watakuwa na kibarua cha kujaribu kufuzu kucheza fainali za wachezaji wachezao ligi za nyumbani yaani CHAN. Jumapili watakuwa ugenini Kigali kujaribu kuwafunga wenyeji AMAVUBI ili wafuzu. Lakini mie naona kama tushafungwa mechi hii kwa sababu kila kona watu wameipa kipaumbele mechi ya 'kishkaji' na Brazil kuliko mechi ya mashindano na Rwanda. Sijamsikia mtu akipanga mikakati ya kuwafunga Rwanda. Naisikia mikakati ya kulipa kiingilio cha malaki kuwaona wachezaji wa Brazili wakibadilishana jasho na wa kwetu. Nadhani hata wachezaji wa Stars wanasubiria mechi ya Brazil zaidi kuliko ya Rwandwa. Yangu macho lakini nawapa Rwanda 80% kufuzu

Labels:

1 Comments:

At 3:59 AM, Blogger Fadhy Mtanga said...

Kinachonikera ni kitendo cha tifua tifua kuona mechi ya Brazil ndiyo muhimu kwetu kuliko ya Amavubi.. Tutafungwa vizuri kabisa. Sitafuni maneno hapa.

 

Post a Comment

<< Home