Thursday, February 17, 2011

SAFARINI MATAMBA
Jana siku Kuu ya Maulid mimi na waminifu wangu tuliona tukaisherehekee kijiji cha Matamba wilayani Makete. Sio mbali sana na Mbeya Mjini. Ukiwa unaelekea Iringa unachepukia Chimala kuelekea milimani. Ni Milima iliyo mikali huwezi kudhani kuna hata barabara huko



Hapa ni katikati ya safari yetu. Chini kule chini ndio mji wa Chimala. Hatuko kwenye ndege ama helikopta. Kwa mbali unaweza kuona barabara iendayo katika mashamba ya mpunga ya usangu. Pia unaweza kuona mashamba ya mpunga.


Ukifika Matamba shurti upozee koo. Ulanzi huo. So sweeet.
Ukiwa Matamba unakuwa karibu kabisa na vivutio vya kitalii kama ziwa Ngozi na Hifadhi ya taifa ya Kitulo. Huko tutafika siku zingine



Safari ya kurudi. Chimala kuleeeeeee mbali.em>


Waaminifu wangu (shoto na kati)na dereva wetu (kulia).

Labels:

5 Comments:

At 10:17 AM, Blogger Fadhy Mtanga said...

kaka bila shaka mlikuwa na wakati mzuri sana kwa kiwango cha kutosha tu. vipi baridi huko milimani?
ahsante sana kwa kutushirikisha hili. nami nimefaidi sana kuiona Chimala kwa mbali.

 
At 10:32 AM, Blogger kassim said...

Huo ulikuwa ni mkangafu au mdindifu?

 
At 12:21 PM, Blogger Goodman Manyanya Phiri said...

Milima!

Mara baridi!

Sasa ni ulanzi!

Mbuga za wanyama!

Hongera sana, Mkuu!


Mimi na amini:
"Kipenda roho hula nyama mbichi!"

 
At 1:30 AM, Blogger Simon Kitururu said...

Duh! Hiyo kitu ULANZI sijatesti longi kweli yanin kwa kuangalia tu mdadi umepanda! Ngojea nikapooze mdadi na BIA tu sasa ntafanyaje?:-(

 
At 1:46 AM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Mliinjoi sana kwa kweli, si wengi hupata wazo la kusherehekea sikukuu Kiutalii. Mandhari nzuri sana.

Kila la heri.

 

Post a Comment

<< Home