Wednesday, February 23, 2011

DOWANS KAPIGWA PICHA !!!
Mmiliki wa kampuni inayosemwa kutaka kuidhoofisha mifuko ya watanzania, Brig. Jenerali Sulaiman Mohamed yahya Al-Adawi aliripotiwa kukataa kupigwa picha.
Jana majamaa yamemtwanga picha akikagua "asset"zake.

HIVI KWA NINI AJIFICHE?

Labels:

6 Comments:

At 1:41 AM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Hata mimi sielewi, kwa nini hataki kujulikana..

 
At 5:29 AM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Mija, lazima atakuwa na sababu kubwa ya kutotaka kujulikana...

 
At 9:07 PM, Blogger Candy1 said...

Mmmmh...ana lake huyo! Sasa alikuwa anaficha nini?

 
At 5:36 AM, Blogger emu-three said...

Duuh!

 
At 7:15 AM, Blogger SIMON KITURURU said...

Kuna watu wengi hawapendi kupigwa picha! Mimi binafsi nawajua wengi hasa kutokana na kuwa huwa sitembei bila kamera mfukoni kwa miaka mingi tu na ni mara kibao hukutana na watu hasa WAISLAMU ambao kwa kIIMANI ambao wao na picha ni mwiko.

Kumbuka kuna waislamu kibao ambao wanaamini PICHA au hata michoro ya watu imekatazwa kwenye kuruani . Ndio kisa Afganistani MATALIBANI walipiga marufuku picha na kubomoa masanamu na vinginevyo vingi.


Pia kuna wasiopenda tu kupigwa picha kisababu zao tu kwa kuwa nakumbuka wakati naishi Sweden enzi duka mtandao la KIJERUMANI liitwalo LiDL linaingia na kutishia kushusha bei za maduka mengine Sweden kwa kuwa linamchezo wakuuza bidhaa kwa bei rahisi kitu ambacho kingeathiri maduka ya wafanya biashara wadogo. Katika Malumbano waliokuwa wanataka kujua ni nani anamiliki LiDL ikagundulika hajawahi kupigwa picha kwa miaka mingi kwa kuwa hataki hicho kitu na picha yake ya mwisho na moja tu kwa wakati huo ilipatikana ilikuwa ni yamiaka ya sabini huko.


Kwa hiyo haya mambo yapo . Na mpaka DADA yangu mzazi ambaye ni wa pili katika familia yetu kumpiga picha ni kasheshe.Na si mmesikia kuna watu wanalala mika kuwa DOWANS inashambuliwa kwa kuwa mmiliki wake anavaa kanzu kwa hiyo sio MKRISTO?

 
At 10:13 AM, Blogger Goodman Manyanya Phiri said...

@Kitururu

Asante sana kwa kutuelimisha.


Wacha sisi sote tuwe PAPARAZZO!

 

Post a Comment

<< Home