Tuesday, February 22, 2011

MAKUBALIANO KIKAO CHA WANA-MALANGALI
Makubaliano haya sio rasmi. Nimetumiwa na mtu aliyekuwako katika kikao kilichofanyika 5/2/2011.Baadhi ya wasomaji wa blogu hii walitaka kujua yaliyojiri huko.Wanafunzi Malangali.

Yafuatayo ni makubaliaono

Hakika kikao kilikuwa kizuri sana, kulikuwa na umati wa 'Wanamalangali' kama 40 hivi. Kamati ya muda ya kuratibu mkutano huo iliteuliwa, ikiongozwa na Stan Nyavanga na wenzake. Walianza kwa kukumbushana mazingira ya sasa ya shule na kuangalia mahitaji ya sasa ya shule yetu.

Makubaliano:
1. Kuunda kamati rasmi ya kutathmini changamoto zinazoikabili shule kwa sasa na kuangalia namna ya kukabili changamoto hizo (ikiwemo kushuka kitaaluma katika maka ya hivi karibuni)

2. Kuunganisha wanafunzi wote waliosoma Malangali kwa njia ya mtandao na njia ya ana kwa ana (ili kuwapa fursa hata wale walio mbali na Malangali) kupata taarifa za mara kwa mara na kuchangia maendeleo ya shule.

3. Kuitisha mkutano mwingine mapema iwezekanavyo ili kuanzisha 'Alumni' ambayo itakuwa na katiba rasmi na uongozi rasmi kwa ajili ya kushughulikia changamoto za shule.

4. Kuwakutanisha wana Malangali angalau mara moja kwa mwaka

5. Kuanza kuchangia ununuzi wa vitabu vya kiada na ziada na kuvikabidhi shuleni kwa utaratibu utakaopangwa, ili kukuza taaluma. Lengo ni kuongeza vitabu ambavyo tumesaidia kuvichakaza kwa elimu tuliyonayo ili wadogo zetu nao waweze kusoma.

Maazimio hayo yatajadiliwa zaidi katika kikao kijacho.

Mwalyoyo

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

<< Home