Thursday, February 23, 2006

Waliochoma Hoteli ya Mpinzani Zanzibar Huru!
Raisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amewasamee watu watatu waliohukumiwa vifungo vya kati ya miaka mitatu na mitano kwa kuchoma hoteli ya mgombea mwenza wa urais wa jamhuri ya muungano kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi, mama Naila Jiddawi. Watu hao wamesamehewa tu kutokana na uwezo alionao Rais wa kumsamehe mfungwa yeyote, uwezo aliopewa na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Kifungu cha 59. Isome vema habari hii hapa.

Sina kinyongo na hawa ndugu walioachiwa lakini Jeff Msangi na wenzio mnaojua sheria nifumbueni mboni hizi nzito kuwa hakuna wafungwa wengine wa makosa kama ya kuiba nyanya waliostahiki kusamehewa hata wakasamehewa hawa ambao sheria iliwanasa kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni 40. Nini kilichofichwa hapa.

Tuesday, February 14, 2006

Hatujachoka tu Kuwa Watazamaji?
Kombe la Mataifa ya Afrika limemalizika juma lililopita kule Misri kwa wenyeji kuwang’oa kwa taabu Ivory Coast. Kama kawaida yetu Wabongo tuliendelea kuwa washabiki wa timu zingine tu kama anavyosema Ndugu yangu Njili Mwakoba hapa. Kwa mara ya kwanza na mwisho Tanzania kushiriki mashindano haya ilikuwa mwaka 1982, tena baada ya nchi nyingine (siikumbuki) kujitoa hivyo bongo kupata chansi baada ya kuishindilia KK-11 (Zambia).

Miaka yote hii sisi tumekuwa watazamaji na washangiliaji wakuu wa Kombe hili, Kombe la dunia (mimi nitakuwa Brazil na Uingereza mwaka huu) na makombe mengine. Freddy Macha amenifanya nitanabahi kuwa kumbe Wabongo ni longolongo tu. Msome mzee Gado hapa uzijue hizo longolongo.

Hivi yawezekana kweli amani (hiyo inayosemwa ipo Bongo) inachangia kudorola katika michezo? Hivi ni kwa nini sisi tumekuwa wasindikizaji tu miaka yote? Macha (Freddy) anahusianisha vita, vurugu na machafuko na mafanikio katika mpira wa miguu.

Afika ya kusini iliibuka kidedea miaka michache baada ya kuchomoka katika ubaguzi wa rangi katika miaka ya 1990. Sasa tuna Angola, Rwanda, Congo ya Kabila na Ivory Coast kama miamba tishio katika soka. Zote hizi ni nchi ambazo zimekuwa zikizipiga ndani kwa ndani. Kumbuka hata hiyo Angola iliingia Kombe la dunia baada ya kuichapa Rwanda kule Kigali. Je yafaa nasi tulianzishe Bongo ili tufanikiwe katika soka? Mungu apishie mbali mbali.

Juhudi zangu za kucheza soka ziligota wakati Fulani huko shuleni. Lakini haina maana kuwa Bongo hatuwezi kuwa na wakina Didier Drogba, Kolo Toure, Jay Jay Okocha, Samuel Etoo, Solomon Olembe, Mark Fish na wengine wenye majina matamutamu katika soka. Wakina Hussein Marsha, Said Mwamba, Edibily Lunyamila Hilary Hemed, Zamoyoni Mogela, Joel Bendera hawakuwa watu wa kufananishwa na hawa ndugu?

Ni nini hasa tunachokosa. Sisi ni masikini sana kuliko haya mataifa mengine ya Afrika? Hata Kenya na Uganda walau ama zinashirikishiriki mashindano makubwa au zinafika mbali kwenye matumaini. Tutakapokuwa na wachezaji sema wanne hivi katika ligi ya Uingereza kwa mfano hata utalii wetu utakuwa maana jina la Bongo (Tanzania) litakuwa linatajwa-tajwa huko kunakotoka pesa. Wito nautoa twende kwa Tekelo (kwa mnayemjua mniambie alikuwa nani) tukapige ramli tumtafute mchawi wetu. Mie nimechoka, sijui wewe.

Hebu watazame Didier Drogba wa Ivory Coast (picha mbili ndogo), Austin Jay-Jay Okocha (katikati) na Lucas Radebe (chini) wanavyojisikia kuwakilisha nchi zao katika ulimwengu wa soka. Sisi ? Pangu Pakavu...

Thursday, February 09, 2006

Hivi Waarabu Watakunywa Maji Yetu Hata Lini Tukiwatazama Tu?

Uzuri wa kuwapo hapa Marekani ni kuweza kupanuka kwa kiasi kikubwa kwa kufikiri kwangu tofauti na pale awali ambapo hata mambo madogo niliweza kujingika kwayo. Pia kuweza kupata vifursa vya kutembelea hapa na pale. Hili la maji nilikuwa nalijua kwa kiasi fulani tu lakini si kwa kiasi nilichonacho sasa hasa ya baada ya kuhudhuria mkutano wa maji Ijumaa 3/ Machi/ 2006 Umoja wa Mataifa New York.

Mkutano huu ulihusu Changamoto za Maji katika Dunia. Ingawaje mkutano huu ulikuwa na wahudhuriaji kutoka jumla ya nchi 128 (Tanzania ikiwakilishwa nami ) watoa mada wengi hawakunivutia walipokuwa wakiongelea ‘Dunia’ wakimaanisha Ulaya na Marekani labda na Japan, China na Mashariki ya kati. Wakati fulani baadhi waligusia Afrika kana kwamba ni nchi moja vile. Wakiongelea vinchi kama Luxemburg ni inchi moja na wakiongelea Afrika eti nayo ni nchi moja. Sijui ni wajinga, mbumbumbu au hamnazo.

Ingawaje mengi yaliyozungumzwa ni mema lakini nilistaajabishwa si tu na watoa mada bali pia na wachangiaji waliopata fursa ya kusomwa maswali ama hoja zao. (Vikaratasi vyangu havikusomwa sijui kwa makusudi au bahati mbaya). Hakuna hata mmoja aliyezungumzia vita ya maji ya Mto Nile.

Kwa kifupi kumekua na kupigana vijembe kwa chinichini hata kutangaza vita baina ya Misri na Sudan kwa upande mmoja na Rwanda, Burundi, Tanzania, Kenya, Uganda, Elitrea, Congo na Ethiopia kuhusu nani hasa ni mmiliki halali wa maji ya Mto Nile.
Mwaka 1929 ililipitishwa Sheria na Uingereza kuwa ni Misri pekee ndiyo yenye mamlaka ya kutumia maji haya. Katu kisijitokeze kinchi kingine kuchimba bwawa au kumwagilia mashamba kutoka vyanzo vya Mto Nile likiwemo Ziwa Victoria.
Mwaka 1959 wakatunga sheria nyingine kuwaunganisha Waarabu wenzao wa Sudan. Sheria hizi za Mwingereza ndizo zinazokataza kuchimba mfereji kutoka ziwa Victoria kupeleka pale Dodoma kwa Miruko na Ana Mtangoo. Marekani inasapoti sheria hizi za kipumbavu kwa sababu tu Misri ni mshirika wake mkubwa katika vita zake za kianaizaya za Mashariki ya Kati. Waweza kusoma sana juu ya mgogoro huu hapa na hapa na hapa.

Swali ninalolileta kwenu huku nikilia kwa mchozi wa damu ni: “Waarabu Watakunywa Maji Yetu Hata Lini Tukiwatazama Tu? Yafaa nini basi tuwe na Ziwa Victoria huku hatuezi kuyaonja mji haya kwa kilimo hata twafa na njaa”
Hasira zangu zikapoa kwa kuzuru sehemu mbalimbali ndani ya majemgo ya UN. Katika picha nisiyokuwemo watazama Wamisri wakineemeka na maji yasiyo yao huku wenye maji tukiteseka kwa kiu, njaa na magojwa yanayoambatana na ukosefu wa maji.

Monday, February 06, 2006

Kikwete Apangua Wakuu wa Mikoa

Rais Jakaya Kikwete amechagua wakuu wapya wa mikoa 11 , kawahamisha 10 waliokuwapo na kuwabakiza Ndugu Yussuf Makamba na Ndugu Anatoli Tarimo Dar es Salaam na Manyara. Katika wapya kuna wanawake watatu. Wapya ni William Lukuvi (Dodoma), Enos Mfuru (Kagera), Saidi Meki Sadiki (Lindi), John Mwakipesile (Mbeya) na Henry Shekifu (Mtwara).
Wengine ni Dk Alex Msekela (Mwanza), Dk Christine Gabriel Ishengoma (Pwani), Brigedia General Dk Johannes Balele (Shinyanga), Moniica Mbega (Ruvuma), Parseko Vicent Ole Kone (Singida) na Mohammed Abdulaziz (Tanga).
Abbas Kandoro amehamishwa kutoka Tabora kwenda Arusha; Jaka Mwambi anakwenda Iringa kutoka Tanga, Halima Kasungu anakwenda Kigoma kutoka Singida na Isidore Shirima anakwenda Mara kutoka Mtwara.
Wengine ni Said Kalembo anayekwenda Morogoro kutoka Ruvuma, Daniel Njoolay anayekwenda Rukwa kutoka Mwanza, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (father Ditto) aliyehamishiwa Tabora kutoka Pwani na Mohamed Babu anayekwenda Kilimanjaro kutokea Arusha .
Walioenguliwa ni Tumainieli Kihwelu (Kagera), Balozi Nimrod Lugoe (Mara), Abubakar Mgumia (Shinyanga), James Luhanga (Iringa), George Mkuchika (Rukwa) na Mateo Qaresi (Mbeya). Pia wamo Stephen Mashishanga (Morogoro), Mussa Nkhangaa (Dodoma), Mahawa (Kigoma), Nicodemus Banduka (Lindi) na Bi Hilda Ngoye (Kilimanjaro).

Sunday, February 05, 2006

Turejee Kwenye Mavazi Haya...Ngumu Eeeh!
Mapacha hawa (pichani) wa kule Zimbabwe wamadhamiria kurejesha heshima ya uafrika, walau kwa kurejea aina za mavazi wanayodai eti waafrika tulikuwa tunayavaa kabla ya bongo zetu kujeruhiwa na utumwa na ukoloni.
Ndugu hawa, Tafadzwanashe na Tapiwanashe Fichani, wameanzisha kampeni kabambe ya kutaka kuwashawishi waafrika wote wavae ngozi za wanyama, vibwaya, shanga na kadhalika. Wasome vizuri hapa. Wao si tu wanasema bali wanafanya hivyo katika kitongoji wanachoishi huko Harare.
Hata hivyo juhudi zao hazijafua dafu kwani waliswekwa rumande kwa majuma mawili na kushitakiwa kwa kutembea uchi. Baada ya kuelemewa na sheria wamelazimika kuacha kuvaa ngozi na vibwaya na sasa watakuwa wanavaa mashati na kaptura.
Wewe ndugu msomaji vipi waonaje tuwaunge mkono hawa majamaa. Tuanze kutembee makalio nje katikati ya mtaa wa Samora. Ngumu kidogo eeeh! Suti, viatu na masweta makali makali ya kutoka London na Paris tumuachie nani?

Thursday, February 02, 2006

Matatizo ya Kiufundi.... We Acha-ga Tu!!!
Kublogu Kwataka moyo. Hivi majuzi nikiwa nahangaika kubandika picha yangu kunako plofile si ndio zikazuka blogu mbili zote zangu; zote 'Baragumu'. Nikaona isiwe tabu. Nikaifuta (delete) ile niliyona imejipendekeza. La haulaa !!!!!!!!!!!! Si nikafuta niitakayo na kuibakiza nisiyoitaka.

Kwa lifupi ile niliyoifuta ndiyo hiyo ambayo wengi wenu mnayo katika viunganishi vyeni. Siwezi ku-log in tena na hivyo basi leo najitangaza mwenyewe kuachana na mke huyo na kumuoa mke huyu. Huyo ananipenda na namuita http://mwaipopo.blogspot.com Ndesanjo, Makene, Da'MiJa na wengine badilisheni kiunganishi chenu.

Alamsiki Binuur

SEHEMU ZA SIRI ZANYIMWA HAKI MAREKANI.
Ndugu yangu David Kiyeu kutoka Kenya, ambaye naye anafundisha Kiswahili Rhode Island hapa Marekani, aliniandikia maono yake haya kuhusu jinsi wamarekani walivyo huria hata sasa wanakengeusha maadili ya kibinadamu ambayo labda hata Mungu anayafagilia kwa sana tu. Kwa kuwa ni mema basi nisipotoshe uhondo ili muusome wenyewe hapo chini:
Haya ndiyo maendeleo wanayojivunia. Ya wanaume kuwa na uhusuano wa kimapenzi na wanaume wenzao. Yashangaza kuwaona wanawake wakikiuka kanuni za kimapenzi; kwamba sharti mwanamke aridhishwe kiu na mwanamume bali sio mwanamke mwenzake. Hii ndiyo demokrasia wanayoizungumzia na kuitangaza kote ulimwenguni. Dhambi ya aina hii imeambukizwa vijana pia huku Marekani na huwezi katu kuwakaripia maanake sheria za nchi zinalinda demokrasia, kama wanavyosema. Unapotazama filamu zao mojawepo ya maudhui ni ngono za jinsia moja.

Inapotukia ngono kati ya mwanamume na mwanamke, mambo yanakuwa ya firauni sasa. Midomo imechukua nafasi ya sehemu za siri ya mwanamke na mwanamume.Yashangaza kusikia jinsi hawa 'walioendelea' ni wachafu hasa katika midomo yao. Mbona mwanamke anyonye shakawa za mwanamume huku mwanamume akipata uhondo katiba kukiramba kile kidude. Ikizidi wataziramba ngoko pia; kunakotokea kinyesi. Nimekuwa makini sana kutompa busu yeyote hapa Marekani maanake sijui dakika chache zilzopita alikuwa akifanya kazi gani na siko tayari kupakwa kinyesi katika shavu langu mie.

Kuna msamiati huku kwa jina sherehe za kimapenzi au kwa king'eng'e wanaziita 'sex parties'. Hapa swala kuu si kuonja vyakula mbalimbali vilivyotayarishwa bali ni kumuonja yeyote yule aliyekuja. Hamna faragha hapa. Ngono zitafanywa wazi sakafuni, kutani, vitandani kwenye makochi n.k. Juzi kumekuwa sherehe hapa chuoni Brown. Waliita sherehe yao 'Gay Students Association'. Ili uweze kukubalika, ulihitajika kuja pale ukiwa uchi au chupi na kanchiri pekee. Nilikuwa pale kushuhudia jinsi 'demokrasia' imekengeusha wanafunzi Wamarekani.

Usimwone binti na ghulamu wamekubatiana ukadhani itakuwa hivi hadi kifo kitakapowatenganisha. Jana binti huyu alikuwa na boifrendi tofauti na juzi na atakuwa tofauti pia ijapo kesho kutwa. Katika ndoa ni vivyo hivyo. Iwapo mwanamume ameanza kulegea basi huenda akaletewa ndume kazi kitandani mwake. Katika matangazo yao utaona tangazo kama hili;

"Mimi na mume wangu tumeamua kuwa na mhusika wa tatu katika ngono. Ningependa
kumtazama mume wangu akifanya ngono na mwanamke mwingine...."

Mniambie Wakristo nikidhani pia Waislamu, je haya yanakubalika katika dini? Licha kwamba wenzetu hawa ni matajiri wa tekinolojia wao ni maskini hohehahe wa kimaadili. Nina uhakika bara la Afrika ndilo linaongoza ulimwenguNI katika kuwa na utajiri mkubwa wa maadili ya jamii.