Tuesday, February 14, 2006

Hatujachoka tu Kuwa Watazamaji?
Kombe la Mataifa ya Afrika limemalizika juma lililopita kule Misri kwa wenyeji kuwang’oa kwa taabu Ivory Coast. Kama kawaida yetu Wabongo tuliendelea kuwa washabiki wa timu zingine tu kama anavyosema Ndugu yangu Njili Mwakoba hapa. Kwa mara ya kwanza na mwisho Tanzania kushiriki mashindano haya ilikuwa mwaka 1982, tena baada ya nchi nyingine (siikumbuki) kujitoa hivyo bongo kupata chansi baada ya kuishindilia KK-11 (Zambia).

Miaka yote hii sisi tumekuwa watazamaji na washangiliaji wakuu wa Kombe hili, Kombe la dunia (mimi nitakuwa Brazil na Uingereza mwaka huu) na makombe mengine. Freddy Macha amenifanya nitanabahi kuwa kumbe Wabongo ni longolongo tu. Msome mzee Gado hapa uzijue hizo longolongo.

Hivi yawezekana kweli amani (hiyo inayosemwa ipo Bongo) inachangia kudorola katika michezo? Hivi ni kwa nini sisi tumekuwa wasindikizaji tu miaka yote? Macha (Freddy) anahusianisha vita, vurugu na machafuko na mafanikio katika mpira wa miguu.

Afika ya kusini iliibuka kidedea miaka michache baada ya kuchomoka katika ubaguzi wa rangi katika miaka ya 1990. Sasa tuna Angola, Rwanda, Congo ya Kabila na Ivory Coast kama miamba tishio katika soka. Zote hizi ni nchi ambazo zimekuwa zikizipiga ndani kwa ndani. Kumbuka hata hiyo Angola iliingia Kombe la dunia baada ya kuichapa Rwanda kule Kigali. Je yafaa nasi tulianzishe Bongo ili tufanikiwe katika soka? Mungu apishie mbali mbali.

Juhudi zangu za kucheza soka ziligota wakati Fulani huko shuleni. Lakini haina maana kuwa Bongo hatuwezi kuwa na wakina Didier Drogba, Kolo Toure, Jay Jay Okocha, Samuel Etoo, Solomon Olembe, Mark Fish na wengine wenye majina matamutamu katika soka. Wakina Hussein Marsha, Said Mwamba, Edibily Lunyamila Hilary Hemed, Zamoyoni Mogela, Joel Bendera hawakuwa watu wa kufananishwa na hawa ndugu?

Ni nini hasa tunachokosa. Sisi ni masikini sana kuliko haya mataifa mengine ya Afrika? Hata Kenya na Uganda walau ama zinashirikishiriki mashindano makubwa au zinafika mbali kwenye matumaini. Tutakapokuwa na wachezaji sema wanne hivi katika ligi ya Uingereza kwa mfano hata utalii wetu utakuwa maana jina la Bongo (Tanzania) litakuwa linatajwa-tajwa huko kunakotoka pesa. Wito nautoa twende kwa Tekelo (kwa mnayemjua mniambie alikuwa nani) tukapige ramli tumtafute mchawi wetu. Mie nimechoka, sijui wewe.

Hebu watazame Didier Drogba wa Ivory Coast (picha mbili ndogo), Austin Jay-Jay Okocha (katikati) na Lucas Radebe (chini) wanavyojisikia kuwakilisha nchi zao katika ulimwengu wa soka. Sisi ? Pangu Pakavu...

10 Comments:

At 3:15 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Nadhani sababu tuko nyuma kisoka ni kuwa "wazee wa kamati ya ufundi" hawapewi maslahi mazuri!

 
At 8:44 AM, Blogger Boniphace Makene said...

Ndesanjo hizo kamati za ufundi una maana za wachawi au makocha? Kuna kazi ya kufanya maana uchawi tumeupa nafasi katika kila kitu ukianza na siasa, masomo, soka, ajira nk kwa mwendo huo tutaishia kupoteza kila mashindano. Lakini Simba si huwa inawakilisha vyema au Baragumu hajui hilo?

 
At 11:17 AM, Blogger John Mwaipopo said...

Bonny nimeandika kuhusu timu ya taifa. Ukitaka andika kuhusu Simba. Hajakukataza mtu.

 
At 4:38 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Nilikuwa ninamaanisha "kamati ya ufundi" na sio kamati ya ufundi!

Makene, simba inawakilisha vyema imewahi kutuletea makombe mangapi ya kimataifa????????????

 
At 8:35 AM, Blogger Indya Nkya said...

Lakini nadhani hatufuati maelekezo ya "kamati yz ufundi" vizuri. Kama uchawi unafanya kazi mimi nadhani tungechukua kombe la dunia. la kufanya ni kumwambia Mchawi ahakikishe kwamba mfungaji anapolenga golini kipa wa timu pinzani anaona mnyama kama simba halafu anakimbia linakuwa goli. Lakini sasa ili hilo lifanyike, ni lazima tuweze kulisogelea goli.

 
At 3:52 PM, Blogger John Mwaipopo said...

Idya: hapo penye kulifikia goli ndio patamu. Vipi Afrika ya Mandela (kusini) siku hizi wameacha kutumia wakina Sangoma. Maana nao wameanza kuwa kama Bongo. Au kwa kuwa wanavitega uchumi vingi Bongo.

 
At 11:35 PM, Blogger Indya Nkya said...

Kaka Afrika ya kusini soka yao imekuwa kama ya bongo. Yaani kuna siasa na ushabiki usio na uvumilivu. Kwa miaka mitatu iliyopita wamebadili makocha mara tatu. Kuna wengine wanasema kwa vile nchi inarudi kwa wenyewe sasa(yaani weusi) basi kila kitu kitaenda mrama!!

 
At 7:17 PM, Blogger January John said...

Asalale!Nasikia tuliwahi fanya kajitihada kidogo miaka hiyo ya themanini tuliposhiriki kombe la mataifa huru.Si kwamba kweli swala la kamati ya ufundi ni tatizo au swala la maslahi.Hata sera zetu za kuendeleza na kukuza vipaji vya michezo ni finyu.Kwa mfano,angalia nchi za Afrika ya Magharibi kama vile Senegal na kwingineko wana shule za kulelea na kukuza vipaji vya soka.Achana na huko mbali, twende kwa jirani zetu Rwanda ambao wameanza na shule ya kukuza vipaji vya soka na FIFA imewapa tafu bila kusahau msaada wa prezida wao.Tukubali kwamba sera za michezo na uongozi wetu havina mwelekeo wa kufufua soka ya mtanzania.Tutaendelea kuwa wa kwanza kutoka mwisho.

 
At 2:28 PM, Blogger MAKALA ZANGU said...

Aisee Baragumu umeongelea maneno ya Mzee Gaddo (longolongo) ila ukibofya unakumbana na jambo jingine. Je unafaham hilo:
http://www.gadonet.com/gcart.asp?w=,108,13,80,137,22,185,20,36,45,63

 
At 9:22 PM, Blogger BIO SLIM HERBAL said...

vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada

 

Post a Comment

<< Home