Thursday, February 02, 2006

SEHEMU ZA SIRI ZANYIMWA HAKI MAREKANI.
Ndugu yangu David Kiyeu kutoka Kenya, ambaye naye anafundisha Kiswahili Rhode Island hapa Marekani, aliniandikia maono yake haya kuhusu jinsi wamarekani walivyo huria hata sasa wanakengeusha maadili ya kibinadamu ambayo labda hata Mungu anayafagilia kwa sana tu. Kwa kuwa ni mema basi nisipotoshe uhondo ili muusome wenyewe hapo chini:
Haya ndiyo maendeleo wanayojivunia. Ya wanaume kuwa na uhusuano wa kimapenzi na wanaume wenzao. Yashangaza kuwaona wanawake wakikiuka kanuni za kimapenzi; kwamba sharti mwanamke aridhishwe kiu na mwanamume bali sio mwanamke mwenzake. Hii ndiyo demokrasia wanayoizungumzia na kuitangaza kote ulimwenguni. Dhambi ya aina hii imeambukizwa vijana pia huku Marekani na huwezi katu kuwakaripia maanake sheria za nchi zinalinda demokrasia, kama wanavyosema. Unapotazama filamu zao mojawepo ya maudhui ni ngono za jinsia moja.

Inapotukia ngono kati ya mwanamume na mwanamke, mambo yanakuwa ya firauni sasa. Midomo imechukua nafasi ya sehemu za siri ya mwanamke na mwanamume.Yashangaza kusikia jinsi hawa 'walioendelea' ni wachafu hasa katika midomo yao. Mbona mwanamke anyonye shakawa za mwanamume huku mwanamume akipata uhondo katiba kukiramba kile kidude. Ikizidi wataziramba ngoko pia; kunakotokea kinyesi. Nimekuwa makini sana kutompa busu yeyote hapa Marekani maanake sijui dakika chache zilzopita alikuwa akifanya kazi gani na siko tayari kupakwa kinyesi katika shavu langu mie.

Kuna msamiati huku kwa jina sherehe za kimapenzi au kwa king'eng'e wanaziita 'sex parties'. Hapa swala kuu si kuonja vyakula mbalimbali vilivyotayarishwa bali ni kumuonja yeyote yule aliyekuja. Hamna faragha hapa. Ngono zitafanywa wazi sakafuni, kutani, vitandani kwenye makochi n.k. Juzi kumekuwa sherehe hapa chuoni Brown. Waliita sherehe yao 'Gay Students Association'. Ili uweze kukubalika, ulihitajika kuja pale ukiwa uchi au chupi na kanchiri pekee. Nilikuwa pale kushuhudia jinsi 'demokrasia' imekengeusha wanafunzi Wamarekani.

Usimwone binti na ghulamu wamekubatiana ukadhani itakuwa hivi hadi kifo kitakapowatenganisha. Jana binti huyu alikuwa na boifrendi tofauti na juzi na atakuwa tofauti pia ijapo kesho kutwa. Katika ndoa ni vivyo hivyo. Iwapo mwanamume ameanza kulegea basi huenda akaletewa ndume kazi kitandani mwake. Katika matangazo yao utaona tangazo kama hili;

"Mimi na mume wangu tumeamua kuwa na mhusika wa tatu katika ngono. Ningependa
kumtazama mume wangu akifanya ngono na mwanamke mwingine...."

Mniambie Wakristo nikidhani pia Waislamu, je haya yanakubalika katika dini? Licha kwamba wenzetu hawa ni matajiri wa tekinolojia wao ni maskini hohehahe wa kimaadili. Nina uhakika bara la Afrika ndilo linaongoza ulimwenguNI katika kuwa na utajiri mkubwa wa maadili ya jamii.

4 Comments:

At 10:46 AM, Blogger boniphace said...

hAYA SASA UNALETA YA KILI TIME HAPA kama umeamua kweli unatakiwa kuandikia makala kuhusu Kili Time kwa Macheni Ohio na kwingine.

 
At 11:49 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Niliwahi kumuuliza mwanablogu Bwaya ambaye aliandika kuwa kushauri watu watumie kondomu kunachochea watu kufanya vitendo vya zinaa. Nilimuuliza, je mambo yanayotokea katika nchi kama Marekani (kama hizo karamu za ngono au ngono za makundi) zinafanyika kutokana na kampeni za kondomu?

Tabia hizi hazitegemei kampeni za kondomu. Chanzo chake ni mambo mengine kabisa.

 
At 5:31 AM, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

whew! umemwaga makala bwana Mwaipopo! kwa ujumla ndio maana nilidhani kuwa dini zilikuwepo ili kudhibiti hiari ya mtu na hisia za mawazo / mwili wake...kwa ufupi kuadabishwa. kwa mfano, mwanamke huvutia kwa mwanamume pia mwanamume kwa mwanamke...binadamu kama wanyama wengine, wanapambana kuexist walisema kuwa mwanaume kuwa na wake wengi ni kanuni ya evolution ili kupanda mbegu nyingi katika maua mengi tofauti ili kusaidia exisence ya human being.......kama nyuki na maua...lakini dini huweka ukomo....

haki za binadamu, zinaanzia kwenye kupigania ukandamizwaji....zinafika kwenye self actualisation (Tanzania tunapigania watu wawe aware) nadhani kupugania demokrasia bora iko kundi hilo.....tukiishazipata ndio inaingia hapo...haki juu ya mwili wako!!!!!! - ndio maana utakuta nchi zilizo hapo ziko kwenjye stage ya juu kabisa kwa uhuru na haki za binadamu.....

sasa basi mungu akapenda tz tukafika hapo....ambapo nafasi ya mungu huwa imeishakuwa kama haipo...maana mungu ni kwa ajili ya sisi wenye vikwazo vingi ambapo hata kupata ugali inabidi mungu aingilie kati.....sijui tuna uwezo wa kuadmit kuwa mungu au kanuni zetu za asili ziendelee kutamalaki??? ciao!

 
At 1:36 AM, Blogger poker said...

PROMO DELIMA
poker online | Agen Domino | Agen Poker|Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | bandar qiu | Judi online terpercaya

Bonus yang kami sediakan :
* TO (Turn over) sebesar 0.3% yang akan di kami bagikan setiap hari senin
* Bonus referal sebesar 10%

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat.
Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: Facebook
Phone number_: +85595678845

 

Post a Comment

<< Home