Thursday, February 02, 2006

Matatizo ya Kiufundi.... We Acha-ga Tu!!!
Kublogu Kwataka moyo. Hivi majuzi nikiwa nahangaika kubandika picha yangu kunako plofile si ndio zikazuka blogu mbili zote zangu; zote 'Baragumu'. Nikaona isiwe tabu. Nikaifuta (delete) ile niliyona imejipendekeza. La haulaa !!!!!!!!!!!! Si nikafuta niitakayo na kuibakiza nisiyoitaka.

Kwa lifupi ile niliyoifuta ndiyo hiyo ambayo wengi wenu mnayo katika viunganishi vyeni. Siwezi ku-log in tena na hivyo basi leo najitangaza mwenyewe kuachana na mke huyo na kumuoa mke huyu. Huyo ananipenda na namuita http://mwaipopo.blogspot.com Ndesanjo, Makene, Da'MiJa na wengine badilisheni kiunganishi chenu.

Alamsiki Binuur

2 Comments:

At 11:23 PM, Blogger mloyi said...

Unajua baragumu hata mimi nina tatizo la kushindwa kutuma picha. Kila siku Mwl Makene ananiambia niweke picha yangu, kwanza nikaiingiza kwenye diskette nikaenda kwenye kompyuta ya bure wakaniambia siruhusiwi kutumia diskette pale. lo nikarudi mitaani nikahangaika kwa masaa kama mawili sikufanikiwa, pesa yangu ikawa imeliwa! nikahangaika hapa na pale, nilipopata kamshahara kangu nikajibana ninunue "flash memory" nikarudi kwenye kompyuta ya bure lakini bado ninahangaika na picha zangu!
Ninavyoona ni rahisi sana kuzituma, angalia makene na ndesanjo walivyojaza picha kwenye ngwangwa zao!,na sio sisi tu tunaohangaika kutuma picha. Sijui tufanye nini kwa hili? Tuwaulize makene na ndesanjo?

 
At 1:33 PM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Mimi pia hata sielewi, kule kwenye ngwanga yangu kila nikiweka viunganishi kesho yake sivikuti, maoni yakiingia siyaoni mara moja ingawa namba inakuwa imejiandika. Sasa hivi NavBar imejikusanya upande mmoja kila nikijitahidi kuirudisha inakataa. Mimi nafikiri kampuni hii itabidi niihame.

 

Post a Comment

<< Home