Monday, February 06, 2006

Kikwete Apangua Wakuu wa Mikoa

Rais Jakaya Kikwete amechagua wakuu wapya wa mikoa 11 , kawahamisha 10 waliokuwapo na kuwabakiza Ndugu Yussuf Makamba na Ndugu Anatoli Tarimo Dar es Salaam na Manyara. Katika wapya kuna wanawake watatu. Wapya ni William Lukuvi (Dodoma), Enos Mfuru (Kagera), Saidi Meki Sadiki (Lindi), John Mwakipesile (Mbeya) na Henry Shekifu (Mtwara).
Wengine ni Dk Alex Msekela (Mwanza), Dk Christine Gabriel Ishengoma (Pwani), Brigedia General Dk Johannes Balele (Shinyanga), Moniica Mbega (Ruvuma), Parseko Vicent Ole Kone (Singida) na Mohammed Abdulaziz (Tanga).
Abbas Kandoro amehamishwa kutoka Tabora kwenda Arusha; Jaka Mwambi anakwenda Iringa kutoka Tanga, Halima Kasungu anakwenda Kigoma kutoka Singida na Isidore Shirima anakwenda Mara kutoka Mtwara.
Wengine ni Said Kalembo anayekwenda Morogoro kutoka Ruvuma, Daniel Njoolay anayekwenda Rukwa kutoka Mwanza, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri (father Ditto) aliyehamishiwa Tabora kutoka Pwani na Mohamed Babu anayekwenda Kilimanjaro kutokea Arusha .
Walioenguliwa ni Tumainieli Kihwelu (Kagera), Balozi Nimrod Lugoe (Mara), Abubakar Mgumia (Shinyanga), James Luhanga (Iringa), George Mkuchika (Rukwa) na Mateo Qaresi (Mbeya). Pia wamo Stephen Mashishanga (Morogoro), Mussa Nkhangaa (Dodoma), Mahawa (Kigoma), Nicodemus Banduka (Lindi) na Bi Hilda Ngoye (Kilimanjaro).

5 Comments:

At 11:37 PM, Blogger Reggy's said...

kuingiza wengi wapya labda hiyo ni sehemu ya ajira 1,000,000 alizoahidi wakati wa kampeni. Lakini mbona wengine amewapunguza kazi? na je mbona amewapa ukuu wa mikoa hata ambao ni wabunge wanne wa kuchaguliwa katika majimbo, eg Lukuvi, Shekifu n.k

 
At 1:26 PM, Blogger boniphace said...

Miruko wewe ndio uko hapo Dom unaweza kutuambia kuhusu hao wabunge kuwa wakuu wa mkoa katika kipindi hiki cha vyama vingi. Kuna makala nimeandikia hilo na kuituma katika safu ya Jumapili nchini kwenye nyumba yetu.

 
At 4:40 AM, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

yeha hata mimi mzozo naunona hapo kwa wakuu wa mikoa kuwa wabunge...au ndio anarudi reverse kubana matumizi?

 
At 2:21 AM, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

Bwana Mwaipopo - mjadala huu niliuanzisha pale kwa Makene kuhusiana na utimuaji wa bwana Siriwa........kuhusiana hoja ya bwana Mwaipopo kumdismiss mheshimiwa mmoja kwa kutohudghuria mikutano imenikumbusha hapbari ya Malawi ambapo raisi Bingu wa Mutharika alipomtimua makamu wake bwana Chilumpha Cassim kwani amekuwa hahudhurii mikutano..japokuwa makamu amedinda mahakamani kuwa impeachment haikufuata process!! Mwaipopo ulipata upinzani wowote? je ulifuata process? ulipata idhini ya SRC au Baraza lenye quorum iliyokuruhusu? ------

 
At 9:23 PM, Blogger Pusat Perkasa said...

vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada

 

Post a Comment

<< Home