Sunday, February 05, 2006

Turejee Kwenye Mavazi Haya...Ngumu Eeeh!
Mapacha hawa (pichani) wa kule Zimbabwe wamadhamiria kurejesha heshima ya uafrika, walau kwa kurejea aina za mavazi wanayodai eti waafrika tulikuwa tunayavaa kabla ya bongo zetu kujeruhiwa na utumwa na ukoloni.
Ndugu hawa, Tafadzwanashe na Tapiwanashe Fichani, wameanzisha kampeni kabambe ya kutaka kuwashawishi waafrika wote wavae ngozi za wanyama, vibwaya, shanga na kadhalika. Wasome vizuri hapa. Wao si tu wanasema bali wanafanya hivyo katika kitongoji wanachoishi huko Harare.
Hata hivyo juhudi zao hazijafua dafu kwani waliswekwa rumande kwa majuma mawili na kushitakiwa kwa kutembea uchi. Baada ya kuelemewa na sheria wamelazimika kuacha kuvaa ngozi na vibwaya na sasa watakuwa wanavaa mashati na kaptura.
Wewe ndugu msomaji vipi waonaje tuwaunge mkono hawa majamaa. Tuanze kutembee makalio nje katikati ya mtaa wa Samora. Ngumu kidogo eeeh! Suti, viatu na masweta makali makali ya kutoka London na Paris tumuachie nani?