Thursday, February 23, 2006

Waliochoma Hoteli ya Mpinzani Zanzibar Huru!
Raisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amewasamee watu watatu waliohukumiwa vifungo vya kati ya miaka mitatu na mitano kwa kuchoma hoteli ya mgombea mwenza wa urais wa jamhuri ya muungano kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi, mama Naila Jiddawi. Watu hao wamesamehewa tu kutokana na uwezo alionao Rais wa kumsamehe mfungwa yeyote, uwezo aliopewa na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Kifungu cha 59. Isome vema habari hii hapa.

Sina kinyongo na hawa ndugu walioachiwa lakini Jeff Msangi na wenzio mnaojua sheria nifumbueni mboni hizi nzito kuwa hakuna wafungwa wengine wa makosa kama ya kuiba nyanya waliostahiki kusamehewa hata wakasamehewa hawa ambao sheria iliwanasa kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi milioni 40. Nini kilichofichwa hapa.

8 Comments:

At 3:53 PM, Blogger boniphace said...

Mwaipopo hapa unafungua mipaka ya nguvu za rais iliyopo katika Katiba. Unanikumbusha Watergate na Nixon maana Nixon alidhani yuko zaidi ya Katiba lakini akajiondoa baada ya kubanwa na majakama. hAPA UNAPATA JIBU KUWA WAFUNGWA HAWA WALITUMWA NA RAIS WA ZANZIBAR KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE ANAHUSIKA NA TUKIO ZIMA. Haya kazi nyingine hiyo nafasi ya demokrasia na tafsiri finyu za Katiba zinavyotumiwa na viongozi wasiotambua mipaka ya kazi zao binafasi na uongozi wa umma.

 
At 9:37 AM, Blogger Jeff Msangi said...

Mwaipopo,
Imesemwa na itaendelea kusemwa kwamba sheria inaweza kuwa kipofu ingawa wakati mwingine huwa inaona kizani.Huu ni mmojawapo wa mifano ambapo sheria huona kizani.Kwanza kwa kutoa adhabu ndogo ambazo hazilingani na makosa na pili matumizi mabaya na ambayo sio ya kiungwana ya watu kama maraisi,makamishna na wengineo.Katika suala kama hili sidhani kama kuna mengi ya kuongelea "kisheria".Ni wazi kwamba kuna faulo imechezwa,kuna dhuluma ya haki imetendeka.Haki haiishi na kupatikana Afrika,nimewahi kuusikia msemo huu.Kwa kumalizia labda niseme madaraka makubwa kwa raisi ni lazima yaangaliwe upya.Wengi wameyarithi kutoka kwa mkoloni.Kwanini hayabadilishwi?

 
At 1:23 AM, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

kwa mara ya kwanza niliposoma habari hii ya kusamehewa hwa wafungwa nikamfananisha bwana Amani Karume na baba yake marehemu Abeid Karume kama nilivomsoma kwenye makala tuliyowekewa na bwana Tungaraza. mzee Karume alikuwa ana uwezo wa kuhuku anavyotaka na akijisikia kupata umaarufu alikwa anakuja gerezani na kutoa msamaha! cha ajabu hakuwa wala si mwanasheria! - ndio maana bado ninasisitiza kuwa inji hizi zina wenyewe na sie ni wasindikizaji!

 
At 3:21 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Kama alivyosema Boni tunaweza kuanza kuhisi kuwa hawa watu walitumwa na serikali ambayo imewasamehe.

 
At 9:14 AM, Blogger Ana said...

Dear John,
I would like to know more about Mrs Naila Jiddawi. Do you know her personally? If so, could I send you an email? Thanks in advance for your help.

 
At 1:29 AM, Blogger John Mwaipopo said...

Justina i happen to know Ms Naila Jidawi as a no nonsense opposition politician in tanzania's achipelago of zanzibar. She was a presidential runnig mate in 2005. i don't know her personally unless i strive to befriend her.

 
At 1:29 AM, Blogger John Mwaipopo said...

Justina i happen to know Ms Naila Jidawi as a no nonsense opposition politician in tanzania's achipelago of zanzibar. She was a presidential runnig mate in 2005. i don't know her personally unless i strive to befriend her.

 
At 9:22 PM, Blogger Pusat Perkasa said...

vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada

 

Post a Comment

<< Home