Thursday, February 09, 2006

Hivi Waarabu Watakunywa Maji Yetu Hata Lini Tukiwatazama Tu?

Uzuri wa kuwapo hapa Marekani ni kuweza kupanuka kwa kiasi kikubwa kwa kufikiri kwangu tofauti na pale awali ambapo hata mambo madogo niliweza kujingika kwayo. Pia kuweza kupata vifursa vya kutembelea hapa na pale. Hili la maji nilikuwa nalijua kwa kiasi fulani tu lakini si kwa kiasi nilichonacho sasa hasa ya baada ya kuhudhuria mkutano wa maji Ijumaa 3/ Machi/ 2006 Umoja wa Mataifa New York.

Mkutano huu ulihusu Changamoto za Maji katika Dunia. Ingawaje mkutano huu ulikuwa na wahudhuriaji kutoka jumla ya nchi 128 (Tanzania ikiwakilishwa nami ) watoa mada wengi hawakunivutia walipokuwa wakiongelea ‘Dunia’ wakimaanisha Ulaya na Marekani labda na Japan, China na Mashariki ya kati. Wakati fulani baadhi waligusia Afrika kana kwamba ni nchi moja vile. Wakiongelea vinchi kama Luxemburg ni inchi moja na wakiongelea Afrika eti nayo ni nchi moja. Sijui ni wajinga, mbumbumbu au hamnazo.

Ingawaje mengi yaliyozungumzwa ni mema lakini nilistaajabishwa si tu na watoa mada bali pia na wachangiaji waliopata fursa ya kusomwa maswali ama hoja zao. (Vikaratasi vyangu havikusomwa sijui kwa makusudi au bahati mbaya). Hakuna hata mmoja aliyezungumzia vita ya maji ya Mto Nile.

Kwa kifupi kumekua na kupigana vijembe kwa chinichini hata kutangaza vita baina ya Misri na Sudan kwa upande mmoja na Rwanda, Burundi, Tanzania, Kenya, Uganda, Elitrea, Congo na Ethiopia kuhusu nani hasa ni mmiliki halali wa maji ya Mto Nile.
Mwaka 1929 ililipitishwa Sheria na Uingereza kuwa ni Misri pekee ndiyo yenye mamlaka ya kutumia maji haya. Katu kisijitokeze kinchi kingine kuchimba bwawa au kumwagilia mashamba kutoka vyanzo vya Mto Nile likiwemo Ziwa Victoria.
Mwaka 1959 wakatunga sheria nyingine kuwaunganisha Waarabu wenzao wa Sudan. Sheria hizi za Mwingereza ndizo zinazokataza kuchimba mfereji kutoka ziwa Victoria kupeleka pale Dodoma kwa Miruko na Ana Mtangoo. Marekani inasapoti sheria hizi za kipumbavu kwa sababu tu Misri ni mshirika wake mkubwa katika vita zake za kianaizaya za Mashariki ya Kati. Waweza kusoma sana juu ya mgogoro huu hapa na hapa na hapa.

Swali ninalolileta kwenu huku nikilia kwa mchozi wa damu ni: “Waarabu Watakunywa Maji Yetu Hata Lini Tukiwatazama Tu? Yafaa nini basi tuwe na Ziwa Victoria huku hatuezi kuyaonja mji haya kwa kilimo hata twafa na njaa”
Hasira zangu zikapoa kwa kuzuru sehemu mbalimbali ndani ya majemgo ya UN. Katika picha nisiyokuwemo watazama Wamisri wakineemeka na maji yasiyo yao huku wenye maji tukiteseka kwa kiu, njaa na magojwa yanayoambatana na ukosefu wa maji.

9 Comments:

At 4:49 AM, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

mwaipopo...kweli nile ina historia....na mgogoro miongoni mwa huo ndio ulipelekea Lowassa kuwa kinara hadi hii nile base management ikaundwa na iko makao yake kenya....nadhani ni kisumu....

tanzania teyari tumevuta maji na niliona salamu walitumiana Egypt na Lowasa kuwa mradi huo hauna madhara kwa giant nile....

maji hayo kwa kweli yameleta kizaa zaa hata waingereza wamekubali. meles zenawi anadai kuwa wafadhili hawataki kusikia habari ya umwagiliaji wa maji.... hata hivyo alikiri kuwa anajua kuwa egypt inafunza askari wa mwituni, na inajulikana huko misri hakuna vichaka....hivyo ni kwa ajili ya mgogoro huu...alinifurahisha kuwa ikiwa misri inataka kuiamulia ethiopia itabidi iitawale, na katika historoa ya dunia hakuna nchi ikawahi kuitawala ethiopia kabla....alitoa wito afrika mashariki kushikiana kwa hili...

http://www.bbc.co.uk/radio4/today/reports/international/watershortage_20050203.shtml

sina reference hapa ila najua hii sheria ya muingereza iliishajadiliwa na pengine ukokotoaji ushanza (kama sie tunaotumia kwa maji kunywa)....cha msingi hapa ni kuwa na matumizi endelevu kwa ajili ya wote....kuna wakati napata hisia labda ndio maana matumizi ya jeshi waliongezeka sana hapa kati kati na manunuzi ya vitu kama rada????

waliogopa kusoma vikaratasi vyako....tunashukuru sana pia kutuwakilisha bila kudai allowansi kwa bidii!!! ndi jinsi pekee tutatokeza pua zetu juu ya maji!!!



cheers

 
At 4:49 AM, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

http://www.bbc.co.uk/radio4/today/reports/international/watershortage_20050203.shtml

 
At 4:51 AM, Blogger FOSEWERD Initiatives said...

nashangaa blog lako halipokei link kikamilifu. nenda www.bbc.co.uk halafu andika meles zenawi nile use halafu search....utaipatya makala nzima

 
At 12:13 PM, Blogger Jeff Msangi said...

Umenifungua macho Mwaipopo,nitalifanyia uchunguzi zaidi suala hili.Naona Mark ameeleza vizuri kuhusu pale tulipo hivi sasa.

 
At 6:12 AM, Blogger mloyi said...

Mungu wao tunampenda lakini maji yetu tunayaona ni yetu tuu!
Tafakari kitu hiki kwa undani.

 
At 3:13 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Mloyi, mchokozi wewe...maji tunasema yetu, ila mungu wao tunamkimbilia. Na majina pia, na kuhiji kwenye vihamba vyao vitakatifu.

 
At 3:44 AM, Blogger Indya Nkya said...

Poa sana Mwaipopo

 
At 11:19 AM, Blogger John Mwaipopo said...

Nashukuru wote

 
At 9:22 PM, Blogger Pusat Perkasa said...

vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada

 

Post a Comment

<< Home