SOKOINE: MIAKA 26 KABURINI
Hayati Edward Moringe SokoineNinapokuwa na nafasi huwa napenda kumkumbuka Hayati Edward Moringe Sokoine kila ifikapo tarehe 12/4, tarehe ambayo royo yake iliuaga mwili. Kwangu Hayati Sokoine atasalia kuwa shujaa wa taifa hili. Kwa kweli kwangu anashika namba ya juu sana. Pengine uadilifu na uaminifu wake ndivyo vilivyowafanya watawala wa miaka ya baadaye wajiaminishe kuwa waziri mkuu bora wa nchi hii atatoka huku alikotoka Sokoine (?). Simply the truest son Tanzania must brag to have had! Wema hawana maisha.
Tarehe kama hii mwaka 2006 nilipata wasaa wa kumkumbuka Hayati Sokoine kwa staili hii hii.
Waweza soma hapa hisia zangu za wakati huo, ambazo zinasalia kuwa hivyo. Hapa chini nawashrikisha michango ya chapisho hili la mwaka 2006:
charahani said...
Mwaipopo
Kwanza umenifurahisha na kauli kuwa anayekaribia kuwa mtakatifu. Sijui protokali za kiromani nasikia sasa hivi eti wapo katika mchakato wa wenye heri halafu wakishamaliza waingie katika huo utukufu. Lakini mhh hivi pamoja na zile operesheni vijiji utakatifu utakuja kweli? (Joke)
Huyu Sokoine kuna bwana mdogo mmoja alizungumza na Bob Makani ambaye aliwahi kuwa naibu Gavana, alimnukuu akisema kuwa Sokoine aliweza kufanya kazi hadi saa tisa usiku hebu angalia hilo.
Inawezekana hili limewafanya viongozi wa sasa kuamini kuwa wamasai ni jasiri hawaogopi mtu ndiyo maana wanafikia sasa mawaziri wakuu wawili kutoka Monduli.
1:56 AM
mwandani said...
Safi Mwaipopo.
Nakumbuka kifo hicho cha Marehemu Sokoine. Nikitoka shule, njiani pale Mikoroshini (siku hizi panaitwa Namanga)nyimbo za polisi na jeshi kote redioni zilikuwa zikipiga. Nakumbuka nilifadhaika, nikasikia uchungu sana.
Hivi karibuni nilitafuta sana habari za Marehemu Sokoine kwenye mtandao nikapata chache tu ambazo hazikueleza kwa kina matendo ya marehemu.
Kumuenzi hayati Sokoine, ingelikuwa vyema kupata habari ndefu na za kina - haswa habari zinazoorodhesha sera zake - kama utekelezaji wa vita dhidi ya wahujumu uchumi... au mengineyo.
3:23 AM
Hudson Eliah Kazonta said...
Mwaipopo,
umefanya kitu muhimu sana kumkumbuka shujaa wetu aliyejitolea kupigana na mafisadi wanaoishambulia nchi yetu kwa kuitafuna kwa kutumia meno yao makali.
ukweli ni kwamba kipindi hicho nilikuwa mtaalam sana wa kulia kila nilipotakiwa kwenda shule kwani ndio nilikuwa nakaribia kufikisha miaka sita tu!
Hongera sana kaka Mwaipopo.
4:31 AM
Boniphace Makene said...
Sfi sana Baragumu, nakupongeza kwa kukumbuka huyu shujaa wetu na pia kupiga hilo dongo nimewcheka sana.
8:36 AM
Michuzi said...
baragumu unatisha! kumbe u wa falsafa hivyo? mie bwana hapa sitii neno zaidi ya kukusifia na kukutonya kwamba kaka wa mama watoto wangu (semkae kilonzo anajua) ameoa hapo monduli, hivyo nasi ni familimemba. kwa kweli ule ni ukoo takatifu, usio na makuu wala majivuno, toka wakati ule yuko hai na hadi sasa. pia ni wasomi wazuri na wachapakazi sana tu. hiyo dhana ya kuwa pm bora lazima atoke huko arusha inaweza kuwa coincidence ama sokoine ali-set precedence nasi tukaizoea hivyo kama hii dhana kwamba kuna ulazima kupeana zamu (bara na visiwani) vipindi vya urais
10:26 AM
Reginald S. Miruko said...
nimekumbuka mengi. Niliwahi kutembelea kaburi lake pale Monduli Juu, takriban km 50 kutoka mjini Arusha, wakati huo ikiwa niaka 12 baada ya kifo chake, nilikuta bado anaenziwa vilivyo, kwani 'KABURI LILIKUWA BADO LINALINDWA NA POLISI WAKATI WOTE'. Sijui sasa hali ikoje.
1:34 AM
tamba said...
Mimi kaka, nakupongeza kwa blogu yako. Nimekuwa mgeni kidogo kwenye nyanja hii na bado natengeneza ya kwangu, lakini tupo wengi na inafurahisha. Nashukuru kwa comment zako kwangu. Usikose kupitia Blogu yangu na napenda maoni zaidi na zaidi
7:23 AM
Ndesanjo Macha said...
Mwaipopo,
Inaelekea kuwa watu kama Morani Moringe wanaweza kuwa wanajitokeza nchini kwetu kila baada ya miaka 200! Ukiachilia mbali kuchapa kwake kazi, ile tabia yake ya kutopenda makuu ilikuwa ya pekee hasa ukiangalia hawa wezi wetu wa siku hizi walioko madarakani. Ingawa operesheni zake hazikuwa na nguvu ya kisheria, nia yake ilikuwa ni kuondoa uchu, uhujumu, na ubadhirifu.
Tufikirie namna gani ambayo watu kama Moringe wanaweza kukumbukwa kwa faida kubwa zaidi kuliko kutumia majina yao kwenye barabara na majengo.
5:21 AM
mwalyoyo said...
Tunakushukuru sana bw Mwaipopo kwa kutukumbusha mtu muhimu sana katika historia ya Tanzania. Nilisoma gazeti fulani makini la kiswahili linalotoka mara moja kwa wiki, kulikuwa na makala moja nzuri sana iliyohusu maisha ya Shujaa Sokoine. Nitajaribu kuwasiliana na wamiliki wa makala ile ili angalau wanablogu wengine waipate kwa njia ya mtandao. Ni jambo la muhimu sana kufahamu historia ya nguli huyu wa Tanzania. Nashukuru kwa maelezo yako ya namna ya kuanzisha blogu, nimeianza na natarajia kuweka habari mbali mbali.
Labels: Wema hawana maisha