Monday, April 19, 2010

WEEKEND MBAYA KWANGU



Awali ilianza kwa kuwaombea njaa Manchester United. But as I was about to celebrate Paul Scholes proved that jealousness never wins with a 30-seconds-to-go header against Man City.



Nikasema haidhuru. Huitaji mwingine afungwe ndipo wewe ushinde. Nikajua tu tutawanyuka Tottenhap Hotspur. Loh! John Terry kwanza akawazawadia penati kisha kama haitoshi 'akatafuta' mikadi iliyomtoa mchezoni.



Nikajipa moyo kuwa haidhuru. Yafaa nini kushabikia ulaya wakati wanangu wenyewe wa Jangwani wangetutoa kimasomaso dhidi ya 'hayawani'. Yale yale ya John Terry, mikadi myekundu miwili tukaipata na kugeuka asusa kwa 'hayawani' wa kariakoo. Pichani kipa wetu Obren Cuckovic akiruka bila mafanikio na kuruhusu goli la kwanza. haidhuru wao wametufunga wakati hamna sikukuu. sisi mwaka jana tuliwafunga wakati wa krismasi

Labels:

3 Comments:

At 9:01 AM, Blogger Fadhy Mtanga said...

Kwani hujui kuna sikukuu ya Muungano? Ama unadhani wote ni Wakatoliki? Kaka pole sana kwa wikendi mbaya kuliko. Sisi Manchester United na Simba Sports Club vijana wetu wamefanya kazi nzuri sana. Ni shangwe tupu.

 
At 2:10 AM, Blogger Alex Mwalyoyo said...

Kazi unayo kaka PF!
Mie ilikuwa raha sana. Huku Scholes anawalaza watoto wa nyumbani na kufufua matumaini ya kugombea kikombe, na huku Mussa Mgosi anawaduwaza watoto wa jangwani na kufukuzia kiatu cha dhahabu! Anyway, ndo mambo yalivyo!

Kazi njema

 
At 4:00 PM, Blogger chib said...

Pole Kaka, ndiyo game hiyo.

 

Post a Comment

<< Home