Thursday, April 20, 2006

Kadhaa au Kadha wa Kadha?
Mtani wangu Marko J Mwipopo (angalia vema jina lake halina 'a', usije fananisha kama wengi wanavyotufananisha)leo amenishitua na mipicha inayonyesha udhalimu unaoendeshwa huko Iran kama unavyoweza kuiona wewe mwenyewe. Ujumbe huu ulikuja na ilani "Kama hautawapelekea wengine picha hizi basi wewe hauna moyo"
Eti kamjaa kakiandaliwa kupewa fundisho
Sijui itauma kama ile njaa?
Uwiiiiii!!!!!!
Aaaaagghhh! isssshhhh!!!!
Kwa mujibu wa maelezo mengine ya picha hizi anayeonekana kuadhibiwa ni kijana wa miaka mi-8 aliyeiba mkate sokoni. Eti kwa sheria za Iran anatakiwa akatwe mkono ili mosi liwe fundisho kwa wengine na pili asiweze kuiba abadani.
Watuma picha wanamalizia kwa kusema "Plead people to stop fighting in the name of religion. To stop doing such deeds, and then justifying them in the name of religion... No religion has ever justified such heneous crime... Pass it on ...let the world know watz happenening in the name of God and religion..."
Baada ya kuziangalia kijuu-juu nikamjibu:
"Thanks for the message at least I am one of the luckiest few to have seen this. I am sorry I am denying others aceess to this story because I have no right to say which religion is good and which is not. It's God Himself. I can see you have been caught by American bandwagon propaganda about Iran. They want to justfy war from all directions. Masuala ya imani yaache tu. Hasn't Christianity, especially Roman Catholicism, done untold and unthinkable harm to the world? Wasn't Bishop Bartolome de las Casas the important figure in history to suggest the yanking Africans to work as slavesin the Americas...
"Imani ziache zilivyo. Mbona walikaa kimya mapadre na maaskofu wa kikatoliki walipokuwa wakichinja watu Rwanda na Burundi. Kama walikuwa bado hawana utu, mbona wako kimya katika vita zinazoendelea Darfur na Congo."
Katika majuma ya hivi karibuni kumekuwa na mkanganyiko hasa Marekani baada ya Iran kutangaza 'kujiunga' katika klabu ya wanaomiliki utundu wa nyuklia duniani, mbali na kuwa ilipembejwa sana hasa na Marekani hiyohiyo hata kutofikiria kujihusisha na teknolojia hii kwani yahatarisha amani ya dunia. Linalofanyika sasa na wamarekani ni kuushawishi uma wa dunia kuwa kuna haja ya kufurumusha Iran, ingawaje wachunguzi wa kivita wanaionya serikali ya Dubya kwenda kimgongo au kitengetenge katika mapigano na Iran. Wanachofanya sasa ni kuiharibu sura nzima ya Iran katika macho ya watazamaji hasa wamarekani maamuma. Pengine mvuvumo huu ndio uliosababisha mimi kumjibu Mwipopo kama hivyo juu.
Wazo lililonijia baada ya kutazama juu-juu picha hizo (kwa undani zinaonekana kama ni danganya toto ya kompyuta tu, mtazamo wangu. Au kwa nini kuna kataulo pale?) nikakumbuka propaganda ambazo Marekani huzipigia baragumu wanapotaka kumuonyesha fulani kuwa ni mbaya. Unakumbuka mwaka 2003 walipotaka kumfurumusha Saddam Hussein walivyotoa msaada mkubwa wa kudhibiti UKIMWE Afrika. Nadhani ilikuwa miongoni mwa juhudi za kuifanya Afrika inyamae na kuiona Marekani na baba bora. Je katika uenezi wa propaganda kama hizi hakuna suala la kadhaa mbali na dini lililojificha hapa?
Mwipopo akanijibu:
"...You have reminded me about the Iran issue now, actually whether we will be affected or not but the middle east is terribly insecure. Anything from now may happen around the region, my worry. Apart from the US's bullying behavior, other countries around theworld are being too extreme to say nothing against the practices of those powers (like Iran)"
Hapa Mwipopo akanipa changamoto mpya tena - kwamba ingawaje Marekani inajipa ukinara ama ukiranja wa kuikemea na kuitisha Irani, kwa nini basi nchi zingine zijajifanya maamuma kabisha kuhusu maendeleo ya nyukilia. Je hatuoni madhara yatakayojitokeza wakati silaha za namna hii zitakapoanza kutumiwa ulimwenguni?
Mwipopo akaendelea kuhusiana na mkanganyiko wa dini, siasa na mauaji ambayo pengine ama dini zinasingiziwa tu ama zinahusika moja-kwa-moja ama si-moja-kwa-moja (indirecly):
Bwana Mwaipopo, mimi nakuunga mkono issue hizi siyo rahisi ku-judge. Lakini nataka nikueleze kuwa tunapotoshwa pia na 'media'. Now I have a real story for example about the killings in Rwanda after, first watching the 'HOTEL RWANDA' movie, and second talking to a catholic student, who is a PhD candidate here, and was a victim of the situation by that time. He says, as a fact of what really happened, there's no priest who by intention or directly caused the killings. And it's a long story about the whole antagonism between the 'white priests' and the government. They were not wanted to be there in other words. Na huyu bwana sasa ni msabato but was raised a catholic from birth to seminary school.
Alamsik Binuur

Wednesday, April 19, 2006

Itazame na Hii Pia
Unataka kusikiliza Sabal Kheri Mpenzi na nyinginezo? Basi kong'oli hapa kisha uburudike, kama unapenda.

Alamsik Binuur

Wednesday, April 12, 2006

Sokoine Kaburini Miaka 22 Sasa
Leo nilipokuwa nafungua kompyuta kuanza kublogu na kutazama kama nimepata barua pepe kutoka Mbeya nikakumbana na habari ya maadhimisho ya miaka 22 ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa vipindi viwili visivyo mfululizo, Hayati Edward Moringe Sokoine (pichani kushoto). Soma habari kwa kukong'oli hapa na hapa.
Sio lengo langu kudhania kuwa hamjui au hamkumbuki kuwa siku ya leo miaka 22 iliyopita Sokoine alikumbwa na mauti kwa ajali ya gari huko Dumila Morogolo akirejea Bongo baada ya kuahirisha kikao cha Bunge. Nilikuwa bado kinda kuelewa siasa za nchi lakini nililia mchozi kwa kusikia nyimbo za maombolezo RTD. Pia waweza jiuliza nini kilimfanya achague usafiri wa gari badala ya ndege iliyokuwa ikimsubiri yeye. Hakika hakuna ajuaye mauti yake yatamfika vipi.
Langu la leo ni kuhuisha kumbukumbu ya kiongozi huyu. Mafikirio yangu ni kuwa pengine alikuwa mhimili mkubwa wa serilali ya hayati (punde kuwa mtakatifu) Rais Julius Nyerere. Nashawishika hivi kwani mwaka mmoja uliofuatia Nyerere aliona yafaa nini kuongoza nchi pasi na 'kamanda' wake. Akang'atuka. Pengine umuhimu wake na utendaji wake wa kazi ndivyo vilivyofanya aenziwe pengine sawasawa na rais mwenyewe hasa katika kubatiza taasisi na viwanja jina lake. (Kuna hospitali ya Sokoine Mtwara, Chuo Kikuu Morogoro na Uwanja wa Michezo nyumbani Mbeya). Hii haikuwa heshima ndogo ati kwa mtu ambaye alikuwa hai bado.
Kwa kifupi natamani kujua hivi huyu mtu alikuwa kiongozi wa namna gani au wa mtazamo gani? Je weledi na uchapaji kazi wake ndio umewapofusha marais wa siku hizi kudhania kuwa "Waziri mkuu bora atatoka Arusha."

Saturday, April 08, 2006

Azimio La Dodoma Linakubalika
Kurunzi (Mwenyekiti), Miruko (Katibu), Mtangoo (Mjumbe) na Kazonta (Mjumbe) hivi karibuni walikutana katika 'Mji Mkubwa' wa nchi ya Tanzania na kujadili na kupitisha kwa niaba ya wamiliki na wachapishaji wa blogu za Kiswahili Azimio. Pamoja na mambo mengine azimio hili linalenga kufungua ukurasa mpya wa uendeshaji wa huduma hii pepe. Pengine wakati fulani tunafikiri na kusahau kuwa kwa kuwa umiliki na uchapishaji wa blogu waweza kufanyika chumbani kwa mhusika huria kabisa basi hata nidhamu, hata ile ya asili tu, haichukui nafasi. Lisome azimio hili vizuri hapa. Wakati umefika sasa wa fikra pevu na endelevu kutamalaki.
Mimi nimeliunga mkono na kulipitisha.

Friday, April 07, 2006

Serikali ya Magazeti na Matapishi ya Ile ya Uwazi wa Kificho
Sijajua sana kuwa ni janja ya serikali kuwapa upya ruksa shirika lisilo la kiserikali la HakiElimu ya kuendelea na shughuli zake za utafiki wa hali ya Elimu Tanzania au vinginevyo. Majuzi waziri wa wizara inayoshugulikia pamoja na mambo mengine elimu, Magreth Sitta, aliwataka HakiElimu waiangukie Serikali (iliyopata umaarufu sana vyumba vya habari) ili waendelee na shughuli zao za utafiti na utoaji hali halisia ilivyo.


(Watoto wamekaa chini huku wenzao wakitanua 'International Schools")

Kesho yake HakiElimu wakasema hawaombi msamaha ng'o kwani walilokuwa wakilifanya ni ukweli na wala si uzandiki kama ilivyodhaniwa na waziri aliyemtangulia katika serikali ya "Uwazi na ukweli" Joe Mungai. Namimi nadhani hivyo pia. Hata hivyo baadhi wa wachambuzi wana mashaka na 'uwazi na ukweli' huo. Msome mzee wa Kitimoto hapa.

Yawezekana kuwa serikali hii yataka kufunika yale mauza-uza ya zama za uwazi na kutoka kivyao. Lakini swali ninalojiuliza kuna haja gani ya kuja kimgongo kama anavyokuja Mage Six. Haitoshi kuwaruhusu tu au ni kutunziana heshima watu wazima. Hivi yale waliyokuwa wakiyasema HakiElimu ni uwongo na uzandiki. Ama Joe alikuwa na lake.

Hebu fikiria jiografia na historia eti vilifanywa somo moja. Huu haukuwa mwanzo wa kuandaa kizazi ambacho kinajua historia na jiografia ya nchi yao nusu nusu. Mfano 'Nyerere' wangemjua kwa jina la 'Nyere', 'Mkwawa' 'mkwa', 'Maji maji' 'maji' . Mungai alikuwa anatupotosha.

Sasa kwenye hili la HakiElimu. Kwa mfano nani asiyejua kuwa badala ya kubukua watoto hufanyishwa shughuli hata zisizo za shule kama kuwachania walimu kuni ama kuwatekea maji. Mjadala waweza kuzuka kuwa elimu ile inamjenga mwanafunzi kuwa mshiriki mwema wa kazi zinazohusu mazingira waliyomo lakini yafaa nini kazi hizo zihamie hata kwa nyumba za walimu. Sijui mliosoma mijini na shule kama za Tanganyika lakini mie maji niliyachota kuni nilizibeba.


(Watoto wakipandisha buku pasi na madawati huku wakiwa hoi kwa mizigo ya kuni)

Swala langu hapa vipi ndani ya siku 100 tu waheshimiwa wanaumbuana namna hii. Yaelekea HakiElimu walikuwa na hoja. Suala ambalo nilikuwa nalipigia upatu. Hoja ya waziri Joe kuwa yapo mazuri ambayo HakiElimu hawayaonyeshi katu haiswihi.Hivi alijisikiaje pale Mage alipokuwa 'akimkanusha' kinamna bungeni. Makene huwa-ga anasema kama kuna mazuri waliyafanya hawapaswi kusifiwa kwani ni wajibu wao. Hebu fikiria kumpongeza mzazi kwa kumpeleka mototo shule. Anafaa asifiwe kwa lipi? Sio wajibu wake? La uongo lipi walilolisema HakiElimu.

Panapo ukweli uwongo hujitenga mithili ya mafuta yajienguapo yachanganyikapo na maji.

Monday, April 03, 2006

Ya Picha Nyingine Hiyooooo
Boniphace Makene amewahi kunidokeza kuwa kijijini anakoishi Mwananchi Communications lazima kuendelee kiblogu-blogu. Amekuwa akiwashawishi wanakijiji wenzake watandae hivi na si haba sasa tuna Yahya Charahani, Morris Mwavizo. Leo asubuni wakati nafungua kompyuta kuangalia huenda nina barua kutoka nyumbani nikakutana na mpigapicha wa kijiji hiki Mpoki Bukuku 'naye amekata shauri'. Kong'oli hapa 'ukamsilimishe'. Hala hala lakini kweni ni mbabe kwelikweli.