Monday, May 23, 2011

KICHWA CHA HABARI

Huku ku-balansi vichwa vya habari magazetini sasa balaa.




Majira Ijumaa Mei 20

Labels:

6 Comments:

At 8:26 AM, Blogger Subi Nukta said...

Kweli kuna kulipua kwa haraka hasa kwa sisi wenye blogu/tovuti kwa kuwa tunaandika na kuendelea na shughuli nyingine zilizotuajiri, sasa hawa ambao kazi yao ndiyo hii waliyoajiriwa nayo, wanashindwa vipi kuihakiki bwana? Maana tofauti kabisa na ilivyokusudiwa. Wawe makini zaidi katika kuhakiki.

 
At 5:57 PM, Blogger Goodman Manyanya Phiri said...

Nilipokuwa nasomea uandishi wahabari mwaka 1991, Mwalimu wangu Anthony Ngaiza alituhadithiya matatizo aliemkumba mhariri mmoja aliekusudia kuandika "Idi Amin Rapped Nyerere" kwa wakati ule wa vita vya kumng'oa jamaa huyo madarakani.

Nasikia alifukuzwa kazi Dar, na alinusurika kupigwa vibaya na wale wanaempenda Mwalimu; kwani yeye badala ya 'raPPed' yeye kaandika 'raPed' jamaani!

 
At 12:47 AM, Blogger John Mwaipopo said...

hii ndio sababu nashindwa kuacha kublogu. hivi ningeyajuaje haya ya 'rap' na 'rape'.

ningekuwa mwandishi wala hata nisingesubiri kufukuzwa. ningejiondokea.

ningekuwa rais nyerere ningemsamehe tu kwa kuwa nyerere alikuwa anajua lugha lakini ningekasirika. ila hofu yangu (yaani kama ningekuwa nyerere)ingekuwa kwa waramba viatu wangu. hawana-ga dogo ati!

 
At 12:53 AM, Blogger Subi Nukta said...

John, wewekama mimi, kabisa nikifikiria kuwa nitaacha kublogu, najiona kama nitapungukiwa njia mojawapo ya kujifunza mambo.

Nisingejua historia ya mwandishi kuandika kichwa cha habari ndivyo sivyo enzi za Nyerere kama siyo Goodman kutoa mfano na kama siyo wewe kutoa kipande kilichokosewa. Ungeamua kupuuzia ukasogoa na wa mtaani tu, sisi tusiokuwa kwenye kilinge cha mtaa wako tungepata vipi elimu ya Goodman?

Goodman asante kwa kutoa mfano wako, maana ungekuwa kimya sijui mi ningejifunza nini hiyo historia na kumbukumbu muhimu.

Blogu elimishi na zidumu daima dumu!

 
At 8:12 AM, Blogger kijiwechahabari said...

hi mambo vp john. hop ya duin good. naomba tufanye kazi pamoja kwa kuwa hata mie ni bloger. check ma blog on www.ngumij.blogspot.com and u may conntact me via 0715992038 or 0686897007 tuone namna gani tunaweza kusonga. mie niko Dsm. asante

 
At 3:15 PM, Blogger Goodman Manyanya Phiri said...

Yote ninayeyaporomosha hapa nimejifunza kwenu, Watanzania kama taifa.

Mwendelee tu wala msichoke kulipenda Bara lenu na watoto wake; hata mkifukuzwa na kupigwa viboko vya moto hapa bondeni kwetu kutokana na XENOPHOBIA ya wajinga wachache!

 

Post a Comment

<< Home