Tuesday, May 10, 2011

HONGERA DA'MIJA KUBLOGU MIAKA SITA

Nimepekenyua blogu zetu za Kiswahili (Tanzania) na kugundua blogu ya Da'Mija Shija Sayi (pichani) imetimiza miaka sita juzi tarehe 8. Huyu mdada ni miongoni mwa ma-bloga wa kitanzania wa kwanza kabisa(Pengine zile 10 za kwanza yumo. pengine).
Da'Mija mwenyewe enzi hizo

Blogu yake ni kongwe kuliko hata ya Michuzi na nyingine nyingi. Huu hasa ndio wakati huwa nauita kwa kimombo 'when blogs were really blogs'. Hapa chini ni sehemu ya hodi yake


"Ngo...ngo..ngo... hodiii, jamani wenyewe mpoo?...inaelekea wametoka, ngoja niache ujumbe mlangoni.

Wanablogu,
Nilipita kwenu lakini inaelekea hamkuwepo, nia hasa ilikuwa nikuwapa taarifa kwamba nami nimeingia katika ulimwengu wa blogu..."HONGERA MWANAKWETU

Labels:

2 Comments:

At 8:27 AM, Blogger Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hongera Da Mija. Songa mbele....

 
At 12:11 AM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Hongera sana sana sana Da┬┤Mija na uzidi kusonga mbele tupo nyuma yako....

 

Post a Comment

<< Home