Sunday, February 14, 2010

MIAKA MI-4 YA SAUTI YA BARAGUMU
Nimekuwa kimya kwa takribani majuma mawili hivi. Nilikuwa Morogoro nikiwatumikia watu asubuhi mpaka saa moja jioni. Uchovu na kuwa mbali na mtandao vilinifanya nishindwe kublogu. Nimerejea kublogu ingawaje bado niko njiani kurudi mbeya. (Niko Dar kutoka Morogoro kwenda Mbeya - imekaaje hii??)

Nikiwa huko Moro Sauti ya Baragumu ilitimiza miaka Mi-4 toka lianzeshwe Februari 2006, New Jersey, USA. Angalia Post nilizoanza nazo wakati huo hapa. Miaka inaenda kasi mmno. Pichani ni picha niliyojipiga nikiwa hotelini Morogoro nikiwa na kashati kangu ka njano nilikokuwa nako wakati naanzisha blogu hii. nakaita kashati ka blogu.

Labels: ,

12 Comments:

At 3:12 AM, Blogger Fadhy Mtanga said...

Kaka ulichoniacha hoi ni kwamba upo Dar ukiwa njiani kutoka Moro kwenda Mbeya. Bahati mbaya enzi zangu za ubaharia pale Jografia sikukaa sana na nilipita usiku. Vinginevyo ningekuwa na uwezo kubeba ndwika hii hoja. Kaka hongera sana kwa miaka 4 o'clock ukiwa unawakilisha fijo.
Na kashati kako uliko jumlishiwa pale Dox kana rangi ya yeboyebo si utani.
Sasa na kabaridi ka pale Mafiat pale Mbeya Carnival unalazimika kukanunulia kajaketi ili usipigweko na baridi chali.
Ukiwa zako njiani kurudi kukaja kwa barabara inayopitia kwanza Ubungo, napenda kukutakia kila la heri kwenye kasikukuu haka tulikokakopi na kukapesti kutoka wuulaya.
Bila shaka uli nu nkasi gwako hapo mna wakilisha kwa matakapera na matopetope na mbalaga za kutosha. Ena, naloli kabisa.
Kawaponiage wooote ukirudi kukaja. Ukamponiage Mwambusi, Mwakatapanya, Mwakasumi, Mwamakula, Mwakalobo, Mwakatobe, Mwakalebela, Alinanuswe, Alimosa, Anyitike, Asangaliswe, Anangisye, Andendelisye, Alinanuswe na woooooote.

 
At 4:09 AM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Shukrani kama umerudi, na hongera blog ya SAUTI YA BARAGUMU kwa kutimiza miaka minne. Kaka John hako kashati hakaishi...lol

 
At 6:33 AM, Blogger Candy1 said...

Happy Birthdaaaaaay!!! Kumbe kaka yangu ni mkongwe kwenye hivi vitu :-). Congrats dear!

 
At 12:28 AM, Blogger chib said...

Hongera kwa blog yako kumaliza umri wa chekechea, sasa inaanza primary wakati zetu bado zipo kwenye level ya kujifunza kutembea!
Kila la heri mkuu

 
At 2:37 AM, Blogger mumyhery said...

hongera sana, kaza buti safari ndio kwanzaaaaaaaa imeanza!!!!!!!

 
At 5:40 AM, Blogger Lazarus Mbilinyi said...

Kaka,
Hongera sana kwa kutimiza miaka 4 ni kweli kama ni mtoto sasa badala kutambaa anapaa hewani kama dege la KLM.

Hongera sana

 
At 6:16 AM, Blogger mwalyoyo said...

Tuko pamoja mkuu, hongera kwa kutimiza miaka minne!
Kila la heri

 
At 7:33 AM, Blogger Masangu Matondo Nzuzullima said...

Baragumu ni lazima liendelee kuunguruma. Hongera!

 
At 10:34 AM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Yaani miaka inaenda jamani, kama unge au ulipata mtoto huko USA tayari analisakata kabumbu.

Hongera sana.

 
At 5:17 AM, Blogger Bwaya said...

Nakumbuka kusoma posti yako ya kwanza enzi zile za akina Kasri Makene, Mloy, Mzee wa Harakati, Mzee wa Kurunzi Mark Msaki, Jikomboe n.k

Miaka inakimbia. Na kadri inavyokimbia blogu nyingi zinazidi kugeuka mahame na nyinginezo zinageuza maudhui.

Hayo yote ni kwa sababu zilizo nje ya udhibiti. Kwa hivyo, ndugu yangu Mwaipopo, kubaki hewani katika miaka 'mine' hii si jambo jepesi. Nikupe hongera sana kwa kuendelea kuwapo ukumbini.

 
At 4:33 AM, Blogger Mzee wa Changamoto said...

Miaka 4?? Duh!!!
Mie nina mmoja na nusu nakaribia kuikimbia fani.
Kwa asiyejua UGUMU wa ku-blog hataona uimara na UBISHI WAKO KWENYE FANI, lakini sisi tunaohaha kila siku kusaka cha ku-post hapa, taoionja joto ya jiwe.
Tunza shati kaka tulione mwakani. Kuweza kulivaa shati ililoanzia nalo ku-blog kunadhihirisha mambo mambo mawili (kama sio moja kati ya haya mawili).
Ama ulinunua shati kubwa kuliko saizi yako wakati huo (kama unaongezeka) au umeweza ku-maintain mwili wako kwa miaka 4 iliyopita.
Yote juu ya yote yaonesha UNA MIPANGO MAKINI.
Hahahahaaaaaaa
Kila la kheri KAKA

 
At 10:38 AM, Blogger SIMON KITURURU said...

Hongera sana Mkuu! Miye ni miongoni mwa wajao humu tokea uanzishe hiki kijiwe na siachi.

Na sauti ya BARAGUMU iendelee kunguruma daima!

 

Post a Comment

<< Home