Wednesday, February 17, 2010

Remmy Ongala...!!!



Leo nimefurahi kujua kuna blogu inayojishughulisha na muziki wa Tanzania. Hii intaitwa Wanamuziki Tanzania. Anayejishughulisha nayo ni mkongwe/mtaalamu John Kitime. Kwa akina siye tunaopenda muziki hasa wa zamani, ambao huwa tunafikiri dunia ya muziki ilishaisha na ujio wa bongo fleva, hapa tumefika. kuna historia, uchambuzi na ufaanuzi mkuu. hayo ya dk Remmy Ongala utayakuta huko. Asante mzee wa changamoto na mzee wa ukweli John Kitime.

Labels:

Friday, December 05, 2008

Ndanda Kosovo ndani ya Nyumba Tena
Yule Mkongomani aliyetikisa sana anga za Tanzania kwa muziki wa dansi yenye mirindimo ya Ki-Kongo almaarufu Ndanda Kosovo ameibuka kivyengine. Yupo na bendi inaitwa Watoto wa Tembo International. Haya tusubiri nini katuandalia Krisimasi hii. Sie yetu macho na starehe tu wakongo wanaposhindana.

Labels: