Wednesday, February 17, 2010

Remmy Ongala...!!!Leo nimefurahi kujua kuna blogu inayojishughulisha na muziki wa Tanzania. Hii intaitwa Wanamuziki Tanzania. Anayejishughulisha nayo ni mkongwe/mtaalamu John Kitime. Kwa akina siye tunaopenda muziki hasa wa zamani, ambao huwa tunafikiri dunia ya muziki ilishaisha na ujio wa bongo fleva, hapa tumefika. kuna historia, uchambuzi na ufaanuzi mkuu. hayo ya dk Remmy Ongala utayakuta huko. Asante mzee wa changamoto na mzee wa ukweli John Kitime.

Labels:

4 Comments:

At 2:25 AM, Blogger Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli na hiyo picha yake duh! inaonyesha alikuwa kijana kweli mziki wa zamani ni zamani. kumbe tupo wengi.

 
At 6:30 AM, Blogger EDWIN NDAKI said...

Hakika Kitime kaja wazo zuri tupo naye pamoja..

tutafika tu

 
At 7:31 AM, Blogger Dkt. Masangu Matondo Nzuzullima said...

"...Kwa akina siye tunaopenda muziki hasa wa zamani, ambao huwa tunafikiri dunia ya muziki ilishaisha na ujio wa bongo fleva"

Umenifurahisha kwa hitimisho lako hili. Bongo fleva kweli ni kazi kweli kweli. Angalia hata hivyo usije ukaambiwa na wanadot com kwamba umefulia!

 
At 6:37 AM, Blogger chib said...

Mambo ya enzi hizo au zama zetu.

 

Post a Comment

<< Home