Thursday, April 20, 2006

Kadhaa au Kadha wa Kadha?
Mtani wangu Marko J Mwipopo (angalia vema jina lake halina 'a', usije fananisha kama wengi wanavyotufananisha)leo amenishitua na mipicha inayonyesha udhalimu unaoendeshwa huko Iran kama unavyoweza kuiona wewe mwenyewe. Ujumbe huu ulikuja na ilani "Kama hautawapelekea wengine picha hizi basi wewe hauna moyo"
Eti kamjaa kakiandaliwa kupewa fundisho
Sijui itauma kama ile njaa?
Uwiiiiii!!!!!!
Aaaaagghhh! isssshhhh!!!!
Kwa mujibu wa maelezo mengine ya picha hizi anayeonekana kuadhibiwa ni kijana wa miaka mi-8 aliyeiba mkate sokoni. Eti kwa sheria za Iran anatakiwa akatwe mkono ili mosi liwe fundisho kwa wengine na pili asiweze kuiba abadani.
Watuma picha wanamalizia kwa kusema "Plead people to stop fighting in the name of religion. To stop doing such deeds, and then justifying them in the name of religion... No religion has ever justified such heneous crime... Pass it on ...let the world know watz happenening in the name of God and religion..."
Baada ya kuziangalia kijuu-juu nikamjibu:
"Thanks for the message at least I am one of the luckiest few to have seen this. I am sorry I am denying others aceess to this story because I have no right to say which religion is good and which is not. It's God Himself. I can see you have been caught by American bandwagon propaganda about Iran. They want to justfy war from all directions. Masuala ya imani yaache tu. Hasn't Christianity, especially Roman Catholicism, done untold and unthinkable harm to the world? Wasn't Bishop Bartolome de las Casas the important figure in history to suggest the yanking Africans to work as slavesin the Americas...
"Imani ziache zilivyo. Mbona walikaa kimya mapadre na maaskofu wa kikatoliki walipokuwa wakichinja watu Rwanda na Burundi. Kama walikuwa bado hawana utu, mbona wako kimya katika vita zinazoendelea Darfur na Congo."
Katika majuma ya hivi karibuni kumekuwa na mkanganyiko hasa Marekani baada ya Iran kutangaza 'kujiunga' katika klabu ya wanaomiliki utundu wa nyuklia duniani, mbali na kuwa ilipembejwa sana hasa na Marekani hiyohiyo hata kutofikiria kujihusisha na teknolojia hii kwani yahatarisha amani ya dunia. Linalofanyika sasa na wamarekani ni kuushawishi uma wa dunia kuwa kuna haja ya kufurumusha Iran, ingawaje wachunguzi wa kivita wanaionya serikali ya Dubya kwenda kimgongo au kitengetenge katika mapigano na Iran. Wanachofanya sasa ni kuiharibu sura nzima ya Iran katika macho ya watazamaji hasa wamarekani maamuma. Pengine mvuvumo huu ndio uliosababisha mimi kumjibu Mwipopo kama hivyo juu.
Wazo lililonijia baada ya kutazama juu-juu picha hizo (kwa undani zinaonekana kama ni danganya toto ya kompyuta tu, mtazamo wangu. Au kwa nini kuna kataulo pale?) nikakumbuka propaganda ambazo Marekani huzipigia baragumu wanapotaka kumuonyesha fulani kuwa ni mbaya. Unakumbuka mwaka 2003 walipotaka kumfurumusha Saddam Hussein walivyotoa msaada mkubwa wa kudhibiti UKIMWE Afrika. Nadhani ilikuwa miongoni mwa juhudi za kuifanya Afrika inyamae na kuiona Marekani na baba bora. Je katika uenezi wa propaganda kama hizi hakuna suala la kadhaa mbali na dini lililojificha hapa?
Mwipopo akanijibu:
"...You have reminded me about the Iran issue now, actually whether we will be affected or not but the middle east is terribly insecure. Anything from now may happen around the region, my worry. Apart from the US's bullying behavior, other countries around theworld are being too extreme to say nothing against the practices of those powers (like Iran)"
Hapa Mwipopo akanipa changamoto mpya tena - kwamba ingawaje Marekani inajipa ukinara ama ukiranja wa kuikemea na kuitisha Irani, kwa nini basi nchi zingine zijajifanya maamuma kabisha kuhusu maendeleo ya nyukilia. Je hatuoni madhara yatakayojitokeza wakati silaha za namna hii zitakapoanza kutumiwa ulimwenguni?
Mwipopo akaendelea kuhusiana na mkanganyiko wa dini, siasa na mauaji ambayo pengine ama dini zinasingiziwa tu ama zinahusika moja-kwa-moja ama si-moja-kwa-moja (indirecly):
Bwana Mwaipopo, mimi nakuunga mkono issue hizi siyo rahisi ku-judge. Lakini nataka nikueleze kuwa tunapotoshwa pia na 'media'. Now I have a real story for example about the killings in Rwanda after, first watching the 'HOTEL RWANDA' movie, and second talking to a catholic student, who is a PhD candidate here, and was a victim of the situation by that time. He says, as a fact of what really happened, there's no priest who by intention or directly caused the killings. And it's a long story about the whole antagonism between the 'white priests' and the government. They were not wanted to be there in other words. Na huyu bwana sasa ni msabato but was raised a catholic from birth to seminary school.
Alamsik Binuur

14 Comments:

At 4:47 AM, Blogger Christian Bwaya said...

Mwaipopo,
Hawa jamaa zako wanapenda waonekane wao ndio watu na wengine ni vikaragosi. Ni mpaka itakapofika wakati tukawagomea kwamba wametuchosha na wanatukera. Nashangaa kwa nini huondoki huko Mwaipopo?

 
At 8:12 AM, Blogger boniphace said...

imetosha, yametimia, nini huzuni ya maumivu ya binadamu?

 
At 10:10 AM, Blogger Indya Nkya said...

Ama kweli kama adhabu hizi zingelifanya kazi kikamilifu basi kungekuwa hakuna mwizi nchi hizo. Mtoto wa miaka 8!! ni hatari mno.

 
At 1:22 PM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Kweli uchungu wa mwana aujua mzazi (mama)!

 
At 1:28 PM, Blogger Jeff Msangi said...

Hebu subiri kidogo..Marekani hivi sasa wanajiandaa kuivamia Iran..sote tunajua hilo.Nataka kuwa makini ili isije kuwa hizi picha zinatokea pale Pentagon ili uvamizi ukitokea tuwaunge mkono?Kwa kusema hivi sio kwamba nakataa au kuunga mkono adhabu kama hizo sio dhidi ya watoto tu bali hata watu wazima.Napinga kabisa mateso kama haya kwa binadamu wenzetu,ikiwemo na ile ya kuchoma wezi moto na kuua vikongwe kule kwetu.

 
At 2:28 AM, Blogger Christian Bwaya said...

Picha hii si ya kweli. Ninachoamini ni kwamba ni za kutengeneza ili kuweka mazingira muafaka wanapokaribia kutekeleza majambo yao kama kawa. Iran hawajawa wabaya kiasi hiki tunachotaka kuelezwa.

Ninachojiuliza ni lini atatokea mbabe wa hawa jamaa atakayekizimisha kiburi chao? Inawezekana ikawa Iran eeeh?

 
At 2:30 AM, Blogger Vempin Media Tanzania said...

Hivi kwa kukakanyaga mkono haka katoto watakuwa wamekasaidia au kukatia ulemavu wa maisha ambao utasababisha kawe tatizo zaidi kwa jamii. Hii ndiyo aina ya adhabu ambazo hazieleweki mantiki zake ingawa wao waweza kujitetea mpaka kufa!

 
At 2:52 AM, Blogger severine said...

Mimi naweza kusema ni kweli swala la dini tuliache kamalilivyo!Ni kweli kwamba hako katoto katabakia kileam maisha lakini ni iamni yao tufanyeje!Ni ulevi wa kiimani!
Wakati mwingine inakera pale ambapo watu fulani katika hii duni wanajiona kwamba wako sahihi kwa kila kila kitu na wanaweza wakahoji kila kitu katika hii dunia!Kwa mfano wanapoipigi Irani kelele kuhusu utundu wa nuklia wakati wao wanayo mimi sioni mantiki yoyote!Mbona hakuna yoyote ambaye yupo tayari kuhoji mambo yoo!Kwa namna moja au nyingine naona hiyo ni propaganda iliyoanadaliwa ili "kujustify" uvamizi mwingine!Kwa yeyote mwenye mtazamo wa mbali ni kwamba uislamu haujaanza leo na wala watu hawajaanza kukatwa mikono leo!

 
At 6:03 AM, Blogger mloyi said...

Sijui wanafundisha nini wengine, ka-mkaja kanasagwa kimkono chake na gari! inafanana na yule anayepigwa mawe kila mwaka.
jaribu siku moja ukanyagwe na baisikeli ndio utajua machungu aliyoyapata huyo mtoto.
Dunia ingekuwa nzuri zaidi kama vitu kama hivi visingekuwepo.

 
At 5:05 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Umeongelea mengi, lakini hili la Joji Kichaka kuijia juu Irani wakati Irani imezungukwa na nchi zenye nyuklia ni utumbo wa siasa za nje wa Marekani. Siasa ya kubaguabagua. Tazama: ukiwa ni mkimbizi toka Haiti, ukifika Marekani ukakamatwa unarudishwa kwenu. Ukiwa ni mkimbizi toka Cuba mguu wako ukagusa Marekani unakaribishwa kwa kupitia sheria iitwao "miguu mikavu." Sheria hiyo inasema kuwa mkimbizo toka Cuba akikamatwa baharini anarudishwa ila akiwa amefika nchi kavu Marekani hatarudishwa.

China nchi ya kikomunisti, uhuru wa habari na kuabudu na kuwa na vyama vya siasa hakuna. Cuba nayo hivyo hivyo, lakini Cuba imewekewa vikwazo, China inakumbatiwa.

Nikomee hapa kabla sijaingiwa na ghadhabu nikavunja hii kompyuta.

 
At 3:10 AM, Blogger Sultan Tamba said...

Yaani kuna mawili, hizi picha zimenichoma, halafu siamini. Kwa Nahisi ni picha za kutengeneza, si umemuona huyu mtu aliyekaa akivuta sigara? Mbona hajabadilika hata kisogo tangu hatua ya kwanza hadi ya mwisho, goti lake naliona liko vilevile! Hizi ni propaganda za kutaka kuungwa mkono ili waichape Iran. Ubinadamu gani huu? Kila kukicha unawaza kuua watu tu! Picha zimenichoma!

 
At 12:25 AM, Blogger Reggy's said...

Ninakubaliana na Jeff asilimia 200 kwamba picha kama hii si ya kweli, ni kutengeneza, pia kwamba inatengenezwa kuvuta hisia za ulimwengu kuwa Iran ni wabaya. Kumbuka kidogo mambo ya Iraq, yalisemwa mengi kwamba kuna silaha, wametafuta hadi leo hawajaziona, lakini Saddam akaondolewa na kufunguliwa mashtaka, jambo ambalo halikuwa hoja yao ya mwanzo-RSM-

 
At 9:34 PM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Tamba umesema kweli.

 
At 9:39 AM, Blogger MICHUZI BLOG said...

jeff umeniwahi. lakini pia charahani umenikuna, ingawa nasema mdogo wangu tamba kuchoma picha hakupigi rivasi hilo tukio. labda nisema kama makene kwamba ; imetosha, yametimia, nini huzuni ya maumivu ya binadamu?

 

Post a Comment

<< Home