Friday, April 07, 2006

Serikali ya Magazeti na Matapishi ya Ile ya Uwazi wa Kificho
Sijajua sana kuwa ni janja ya serikali kuwapa upya ruksa shirika lisilo la kiserikali la HakiElimu ya kuendelea na shughuli zake za utafiki wa hali ya Elimu Tanzania au vinginevyo. Majuzi waziri wa wizara inayoshugulikia pamoja na mambo mengine elimu, Magreth Sitta, aliwataka HakiElimu waiangukie Serikali (iliyopata umaarufu sana vyumba vya habari) ili waendelee na shughuli zao za utafiti na utoaji hali halisia ilivyo.


(Watoto wamekaa chini huku wenzao wakitanua 'International Schools")

Kesho yake HakiElimu wakasema hawaombi msamaha ng'o kwani walilokuwa wakilifanya ni ukweli na wala si uzandiki kama ilivyodhaniwa na waziri aliyemtangulia katika serikali ya "Uwazi na ukweli" Joe Mungai. Namimi nadhani hivyo pia. Hata hivyo baadhi wa wachambuzi wana mashaka na 'uwazi na ukweli' huo. Msome mzee wa Kitimoto hapa.

Yawezekana kuwa serikali hii yataka kufunika yale mauza-uza ya zama za uwazi na kutoka kivyao. Lakini swali ninalojiuliza kuna haja gani ya kuja kimgongo kama anavyokuja Mage Six. Haitoshi kuwaruhusu tu au ni kutunziana heshima watu wazima. Hivi yale waliyokuwa wakiyasema HakiElimu ni uwongo na uzandiki. Ama Joe alikuwa na lake.

Hebu fikiria jiografia na historia eti vilifanywa somo moja. Huu haukuwa mwanzo wa kuandaa kizazi ambacho kinajua historia na jiografia ya nchi yao nusu nusu. Mfano 'Nyerere' wangemjua kwa jina la 'Nyere', 'Mkwawa' 'mkwa', 'Maji maji' 'maji' . Mungai alikuwa anatupotosha.

Sasa kwenye hili la HakiElimu. Kwa mfano nani asiyejua kuwa badala ya kubukua watoto hufanyishwa shughuli hata zisizo za shule kama kuwachania walimu kuni ama kuwatekea maji. Mjadala waweza kuzuka kuwa elimu ile inamjenga mwanafunzi kuwa mshiriki mwema wa kazi zinazohusu mazingira waliyomo lakini yafaa nini kazi hizo zihamie hata kwa nyumba za walimu. Sijui mliosoma mijini na shule kama za Tanganyika lakini mie maji niliyachota kuni nilizibeba.


(Watoto wakipandisha buku pasi na madawati huku wakiwa hoi kwa mizigo ya kuni)

Swala langu hapa vipi ndani ya siku 100 tu waheshimiwa wanaumbuana namna hii. Yaelekea HakiElimu walikuwa na hoja. Suala ambalo nilikuwa nalipigia upatu. Hoja ya waziri Joe kuwa yapo mazuri ambayo HakiElimu hawayaonyeshi katu haiswihi.Hivi alijisikiaje pale Mage alipokuwa 'akimkanusha' kinamna bungeni. Makene huwa-ga anasema kama kuna mazuri waliyafanya hawapaswi kusifiwa kwani ni wajibu wao. Hebu fikiria kumpongeza mzazi kwa kumpeleka mototo shule. Anafaa asifiwe kwa lipi? Sio wajibu wake? La uongo lipi walilolisema HakiElimu.

Panapo ukweli uwongo hujitenga mithili ya mafuta yajienguapo yachanganyikapo na maji.

8 Comments:

At 3:51 AM, Blogger Vempin Media Tanzania said...

Mwaipopo

Hawa hakielimu walichokuwa wanafanya ni kumuumbua baba mbele ya watoto wake tena wakati ambao hakuwa akitarajia. Ndiyo maana wakajifanya kucharuka tena Joe Mungai kama unavyomwita akaungwa mkono kwa nguvu kabisa na Brazake Ben.

Serikali wakati huo ilikuwa ikijisifu kwa watu eti wamejenga madarasa mengi ya MMEM wakajenga nyumba za walimu, wakawa na walimu wa chap chap sijui tuwaiteje maana wa enzi zile walikuwa wakiitwa UPE.

lakini Hakielimu wakawa wanawaumbua kwa kusema ukweli. Hilo liliwauma kupita kiasi! Na watabadilisha sana maamuzi mengi ya awamu ya tatu. Kama ulivyosema wanakula matapishi yao.

 
At 5:35 PM, Blogger Jeff Msangi said...

Wakati serikali yetu inapeleka kilio chake cha kuwataka wasomi na wananchi wake walio ndani na nje ya nchi kuisadia katika ukombozi wa nchi inachofanya katika mambo kama haya ni kinyume kabisa.Jamani serikali inakosea na ikisahihishwa isione aibu kukubali na kujirekebisha.Hapo ndipo maendeleo ya kweli yatapatikana.

 
At 10:07 PM, Blogger Rama Msangi said...

Tatizo kubwa sana ambalo Watanzania wengi wetu tumejijengea ni kuwa aliyeko juu yako daima ni mkweli na hatakiwi kupingwa. Tumesahau ile misemo ya Mkubwa hakosei bali husahau? au ule wa Bosi (ofisini) huwa hachelewi bali anakuwa hajafika? Hii ndio staili ya maisha tunayoishi na ndio hii hii ambayo wakubwa wetu hawa wanaitumia katika kudumaza akili zetu na maendeleo yetu kwa ujumla.

 
At 11:26 AM, Blogger Christian Bwaya said...

Mwaipopo,
Uchambuzi wako safi sana. Hakuna asiyejua kwamba kwa muda wa miaka kumi iliyopita Elimu ilivurugwa kiasi cha kutosha na kutisha. Mambo yaliyofanywa ukiyafikiri unashindwa kuelewa hivi waliokuwa wanapitisha maamuzi hayo walikuwa katika hali ya kawaida kweli ama ilikuwaje.
Haingii akilini kuona masomo kama Fizikia na Kemia yanaunganishwa kwa kidato cha kwanza na pili halafu masomo hayo hayo yanaunganishwa tena kidato cha tatu!
Haingii akilini eti mtu aliyemaliza kidato cha sita anapigwa brash wiki moja halafu anakabidhiwa jukumu la kumfundisha mwanafunzi darasanai! Ama kweli elimu yetu iligeuka tuisieni!
Niliwahi kusoma utetezi wa Joe kuhusu kufutwa kwa baadhi ya masomo nikashangaa. Huyu bwana anasema eti utafiti wa kutosha ulikuwa umefanyika siku nyingi na kwamba alichokifanya yeye ni kutekeleza utafiti huo! Utafiti gani unaofanyika pasipo kuwashirikisha wadau wote? Watafiti ni akina nani hata wafanye mageuza (sio mageuzi) makubwa namna hii kivyao vyao? Hili ndilo tatizo la "top down structure" ya sirikali iliyopita!
Mage kaonyesha mwelekeo kama ataendelea vivyo hivyo maana kurudisha masomo yaliyokuwa yamefutwa kwa minajili isiyoeleweka ni hatua ya kupongezwa!
Lakini wazo langu ni kwamba wote waliohusika na uharibifu huu wawajibishwe kwa kuwaharibia watoto wetu maisha yao.

Walichokuwa wanakisema HakiElimu, kilikuwa sawa bin ukweli.
Tunahitaji watu zaidi watakaothubutu,kama HakiElimu, kuinyoshea kidole sirikali bila woga.

 
At 7:34 AM, Blogger jakogallo said...

nakubaliana nanyi kwa yote mlio sema lakini jamani tusemeni ukweli haki elimu walizidi.msikatae,MMEM pamoja na makosa mengi wameweza kuwaweka wanafunzi darasani wengi tu.na ada zilisitishwa.idadi ya vitabu kwa wanafunzi zimeboreka si semi kuwa ni safi asilimia mia.Lakini hivi haki elimu kweli kazi yao ni kukosoa tu??Hivi fikirieni unatatizo na unajitahidi kulikabili na kuna vikwamisho hapo njiani kama wala rushwa,wazembe,watu wanaotaka kunufuika n.k.halafu kuna mtu yeye kazi yake ni kukuponda tu hachangii chochote.Mimi sijawahi kusikia haki elimu imefadhili hata semina au mafunzo kwa waalimu ya namna kuboresha ufundishaji,wala sijasikia haki elimu imefadhili hata darasa moja wala hata kumfadhili mwanafunzi mmoja.sasa watu kama hawa wanfaida gani???hivi ni kweli MMEM haikuwa na faida??chukulia mfano NGO zingine kam LHRC.(ile ya sheria na haki za kibinadamu)pamoja na kuwa wanaipinga serikali katika baadhi ya maamuzi yake lakini pia wanatoa msaada wa bure kabisa wa kisheria kwa wananchi wanaohitaji huduma hii na pia wanaendesha mafunzo kwa wananchi,mapolisi,juu ya haki zao akina mama tena vijijini wanagawa vitini,vitabu kiujumla wanasaidia na huwa wanatoa mchango wa maana serikali inapohitaji kufanya jambo la kisheria.lakini hii ya haki elimu kwa kweli imezidi,wajirekebishe wakosoe ndio lakini nao pia waunge mkono juhudi za serikali ambazo zimefanikiwa.Sekta ya elimu ni pana na inahusisha watu wengi saa zingine usimamizi unakuwa mbovu na serikali imefanya juhudi sana lakini niwananchi hao hao wanaoiponda serikali ndio wamepewa majukumu mbalimbali katika serikali na ni hao wanaoihujumu serikali.tusipobadilika kama jamii hata kikwete na mama sitta wake watachemsha.tusidanganyane watanzania tunapenda na kuienzi rushwa.angalia watu tunavyopenda kusifu maendeleo ya watu,mwone jamaa mjanja amepata madaraka juzi lakini anagari,keshanunua nyumba hata kama tunjua kuwa mishahara yake haitoshi kufanya hivi.nyie mlioko huko majuu mtakubaliana na mimi kuwa jamii za wenzetu hawapendi kabisa watu wabadhirifu kwa hiyo ni jamii nzima tuwajibike.kikwete pekee hata weza kwa sababu hafanyi kazi pekee yake wangapi tunawajua kabisa wanakula rushwa lakini bado tunawapa kura kwa sababu tu wametununulia pikipiki,saa zingine blanketi,nk.tusiilaumu serikali tujilaumuni sisi kama wananchi.kama tutachukia rushwa serikali haitakuwa na rushwa na ubadhirifu>

 
At 7:00 AM, Blogger Alex Mwalyoyo said...

Joe Asome Hapa!!!!

Tumeizika elimu, elimu ya kizamani,
Elimu ile haramu, maana ya kikoloni
Imetuishia hamu, kuiga ya ugenini,
Elimu yetu ya sasa yawafaa wananchi....

Huu ni ubeti wa kwanza na ni sehemu tu ya shairi refu lililo katika kitabu cha "Tujifunze Lugha Yetu", kitabu cha saba kilichokuwa kinatumika kufundishia lugha ya Kiswahili kwa darasa la tano katika shule za msingi hapa Tanzania. Ni shairi ambalo lililenga kupiga chini mfumo wa elimu ambao tuliurithi toka kwa wakoloni, ambao kwa kiasi kikubwa haukuwa na manufaa kwa jamii ya Tanzania. Sasa huyu Bwana Joe Mungai kufuta baadhi ya masomo muhimu namna hii likuwa na maana gani? Wengine tungekula wapi (hasa sisi ambao tunaishi kwa kutegemea Jografia na Historia?) Hataki wanetu wasome 'Mkwawa Shujaa' au 'Ndoto ya Kimweri' (Kimwei?)au 'Brown ashika tama'? Historia inatufundisha mambo mengi sana ya watu hawa mashujaa, kwa hiyo ni utovu wa nidhamu kuondoa historia ya nchi katika mfumo wetu wa elimu. Ni mambo mengi tu ambayo yalivurugwa katika mfumo wetu wa elimu, ndio sababu wananchi wengi tulifurahi sana tuliporejeshewa masomo yaliyoondolewa katika mitaala. Hata hivyo bado mama Six ana kazi kubwa ya kufanya katika sekta nzima ya elimu, hapo alipofikia ni sehemu tu ya uozo ulipo wizarani kwake. Sababu hii ndio ilimfanya Mkuu wa nchi wa sasa atamke kuwa elimu si mali ya watu wa wizara, ila ni ya Watanzania wote kwa ujumla wao. Mwenye macho haamibiwi tazama. Watanzania tuamke!

 
At 9:31 PM, Blogger Pusat Perkasa said...

vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada

 
At 9:34 PM, Blogger Pusat Perkasa said...

vimax Asli
vimax Asli
vimax Asli
vimax Asli
vimax Asli
vimax Asli
vimax Asli
vimax Asli
vimax Asli
vimax Asli
vimax Asli
vimax Asli
vimax Asli
vimax Asli
vimax Asli
vimax Asli

 

Post a Comment

<< Home