Wednesday, April 12, 2006

Sokoine Kaburini Miaka 22 Sasa
Leo nilipokuwa nafungua kompyuta kuanza kublogu na kutazama kama nimepata barua pepe kutoka Mbeya nikakumbana na habari ya maadhimisho ya miaka 22 ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania kwa vipindi viwili visivyo mfululizo, Hayati Edward Moringe Sokoine (pichani kushoto). Soma habari kwa kukong'oli hapa na hapa.
Sio lengo langu kudhania kuwa hamjui au hamkumbuki kuwa siku ya leo miaka 22 iliyopita Sokoine alikumbwa na mauti kwa ajali ya gari huko Dumila Morogolo akirejea Bongo baada ya kuahirisha kikao cha Bunge. Nilikuwa bado kinda kuelewa siasa za nchi lakini nililia mchozi kwa kusikia nyimbo za maombolezo RTD. Pia waweza jiuliza nini kilimfanya achague usafiri wa gari badala ya ndege iliyokuwa ikimsubiri yeye. Hakika hakuna ajuaye mauti yake yatamfika vipi.
Langu la leo ni kuhuisha kumbukumbu ya kiongozi huyu. Mafikirio yangu ni kuwa pengine alikuwa mhimili mkubwa wa serilali ya hayati (punde kuwa mtakatifu) Rais Julius Nyerere. Nashawishika hivi kwani mwaka mmoja uliofuatia Nyerere aliona yafaa nini kuongoza nchi pasi na 'kamanda' wake. Akang'atuka. Pengine umuhimu wake na utendaji wake wa kazi ndivyo vilivyofanya aenziwe pengine sawasawa na rais mwenyewe hasa katika kubatiza taasisi na viwanja jina lake. (Kuna hospitali ya Sokoine Mtwara, Chuo Kikuu Morogoro na Uwanja wa Michezo nyumbani Mbeya). Hii haikuwa heshima ndogo ati kwa mtu ambaye alikuwa hai bado.
Kwa kifupi natamani kujua hivi huyu mtu alikuwa kiongozi wa namna gani au wa mtazamo gani? Je weledi na uchapaji kazi wake ndio umewapofusha marais wa siku hizi kudhania kuwa "Waziri mkuu bora atatoka Arusha."

10 Comments:

At 1:56 AM, Blogger mzee wa mshitu said...

Mwaipopo

Kwanza umenifurahisha na kauli kuwa anayekaribia kuwa mtakatifu. Sijui protokali za kiromani nasikia sasa hivi eti wapo katika mchakato wa wenye heri halafu wakishamaliza waingie katika huo utukufu. Lakini mhh hivi pamoja na zile operesheni vijiji utakatifu utakuja kweli? (Joke)

Huyu Sokoine kuna bwana mdogo mmoja alizungumza na Bob Makani ambaye aliwahi kuwa naibu Gavana, alimnukuu akisema kuwa Sokoine aliweza kufanya kazi hadi saa tisa usiku hebu angalia hilo.

Inawezekana hili limewafanya viongozi wa sasa kuamini kuwa wamasai ni jasiri hawaogopi mtu ndiyo maana wanafikia sasa mawaziri wakuu wawili kutoka Monduli.

 
At 3:23 AM, Blogger mwandani said...

Safi Mwaipopo.
Nakumbuka kifo hicho cha Marehemu Sokoine. Nikitoka shule, njiani pale Mikoroshini (siku hizi panaitwa Namanga)nyimbo za polisi na jeshi kote redioni zilikuwa zikipiga. Nakumbuka nilifadhaika, nikasikia uchungu sana.
Hivi karibuni nilitafuta sana habari za Marehemu Sokoine kwenye mtandao nikapata chache tu ambazo hazikueleza kwa kina matendo ya marehemu.
Kumuenzi hayati Sokoine, ingelikuwa vyema kupata habari ndefu na za kina - haswa habari zinazoorodhesha sera zake - kama utekelezaji wa vita dhidi ya wahujumu uchumi... au mengineyo.

 
At 4:31 AM, Blogger ARUPA said...

Mwaipopo,

umefanya kitu muhimu sana kumkumbuka shujaa wetu aliyejitolea kupigana na mafisadi wanaoishambulia nchi yetu kwa kuitafuna kwa kutumia meno yao makali.

ukweli ni kwamba kipindi hicho nilikuwa mtaalam sana wa kulia kila nilipotakiwa kwenda shule kwani ndio nilikuwa nakaribia kufikisha miaka sita tu!

Hongera sana kaka Mwaipopo.

 
At 8:36 AM, Blogger boniphace said...

Sfi sana Baragumu, nakupongeza kwa kukumbuka huyu shujaa wetu na pia kupiga hilo dongo nimewcheka sana.

 
At 10:26 AM, Blogger MICHUZI BLOG said...

baragumu unatisha! kumbe u wa falsafa hivyo? mie bwana hapa sitii neno zaidi ya kukusifia na kukutonya kwamba kaka wa mama watoto wangu (semkae kilonzo anajua) ameoa hapo monduli, hivyo nasi ni familimemba. kwa kweli ule ni ukoo takatifu, usio na makuu wala majivuno, toka wakati ule yuko hai na hadi sasa. pia ni wasomi wazuri na wachapakazi sana tu. hiyo dhana ya kuwa pm bora lazima atoke huko arusha inaweza kuwa coincidence ama sokoine ali-set precedence nasi tukaizoea hivyo kama hii dhana kwamba kuna ulazima kupeana zamu (bara na visiwani) vipindi vya urais

 
At 1:34 AM, Blogger Reggy's said...

nimekumbuka mengi. Niliwahi kutembelea kaburi lake pale Monduli Juu, takriban km 50 kutoka mjini Arusha, wakati huo ikiwa niaka 12 baada ya kifo chake, nilikuta bado anaenziwa vilivyo, kwani 'KABURI LILIKUWA BADO LINALINDWA NA POLISI WAKATI WOTE'. Sijui sasa hali ikoje.

 
At 7:23 AM, Blogger Sultan Tamba said...

Mimi kaka, nakupongeza kwa blogu yako. Nimekuwa mgeni kidogo kwenye nyanja hii na bado natengeneza ya kwangu, lakini tupo wengi na inafurahisha. Nashukuru kwa comment zako kwangu. Usikose kupitia Blogu yangu na napenda maoni zaidi na zaidi

 
At 5:21 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Mwaipopo,
Inaelekea kuwa watu kama Morani Moringe wanaweza kuwa wanajitokeza nchini kwetu kila baada ya miaka 200! Ukiachilia mbali kuchapa kwake kazi, ile tabia yake ya kutopenda makuu ilikuwa ya pekee hasa ukiangalia hawa wezi wetu wa siku hizi walioko madarakani. Ingawa operesheni zake hazikuwa na nguvu ya kisheria, nia yake ilikuwa ni kuondoa uchu, uhujumu, na ubadhirifu.

Tufikirie namna gani ambayo watu kama Moringe wanaweza kukumbukwa kwa faida kubwa zaidi kuliko kutumia majina yao kwenye barabara na majengo.

 
At 6:48 AM, Blogger Alex Mwalyoyo said...

Tunakushukuru sana bw Mwaipopo kwa kutukumbusha mtu muhimu sana katika historia ya Tanzania. Nilisoma gazeti fulani makini la kiswahili linalotoka mara moja kwa wiki, kulikuwa na makala moja nzuri sana iliyohusu maisha ya Shujaa Sokoine. Nitajaribu kuwasiliana na wamiliki wa makala ile ili angalau wanablogu wengine waipate kwa njia ya mtandao. Ni jambo la muhimu sana kufahamu historia ya nguli huyu wa Tanzania. Nashukuru kwa maelezo yako ya namna ya kuanzisha blogu, nimeianza na natarajia kuweka habari mbali mbali.

 
At 9:31 PM, Blogger Pusat Perkasa said...

vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada
vimax canada

 

Post a Comment

<< Home