Saturday, April 08, 2006

Azimio La Dodoma Linakubalika
Kurunzi (Mwenyekiti), Miruko (Katibu), Mtangoo (Mjumbe) na Kazonta (Mjumbe) hivi karibuni walikutana katika 'Mji Mkubwa' wa nchi ya Tanzania na kujadili na kupitisha kwa niaba ya wamiliki na wachapishaji wa blogu za Kiswahili Azimio. Pamoja na mambo mengine azimio hili linalenga kufungua ukurasa mpya wa uendeshaji wa huduma hii pepe. Pengine wakati fulani tunafikiri na kusahau kuwa kwa kuwa umiliki na uchapishaji wa blogu waweza kufanyika chumbani kwa mhusika huria kabisa basi hata nidhamu, hata ile ya asili tu, haichukui nafasi. Lisome azimio hili vizuri hapa. Wakati umefika sasa wa fikra pevu na endelevu kutamalaki.
Mimi nimeliunga mkono na kulipitisha.

3 Comments:

At 5:39 AM, Blogger Reggy's said...

Mwaipopo asante kwa kutupongeza na kututia moyo. Nakupongeza pia kwa kuwa msomaji na mchangiaji mzuri katika kila blogu ninayofungua. Keep it up

 
At 12:26 AM, Blogger mzee wa mshitu said...

Mwaipopo

Hili azimio kwa hakika ni la kihistoria kumbuka maazimio ya Tabora na Arusha na kwingineko yaliyotolewa na Mwalimu Nyerere alianza hivi hivi halafu baadaye kila mmoja akawa anarejea maamuzi yake na wenzake hivyo Reginald na wenzake wamefanya kazi kubwa inayostahili kuigwa na wanablogu wengine kokote kule Duniani.

 
At 11:50 AM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Mwaipopo, inafurahisha kuona jinsi ambavyo wanablogu wamelipokea azimio hili kwa mikono miwili. Sijui kama akina Miruko na wenzake wanajua kuwa wametugusa sana kwa kuamua kuja na azimio hili mapema asubuhi asubuhi. Tuliweke kwenye viuongo vyetu. Na tuendelee kulijadili.

 

Post a Comment

<< Home