Wednesday, May 12, 2010

MSAADA TUTANI


Wababe wa Ligi Kuu ya Uingereza wakijinafasi na kombe lao

Ikiwa ni juma la kusherehekea ushindi wa Chelsea wa Ligi Kuu ya Uingereza (najua huu sio wimbo mzuri kwa Chib na Fadhy Mtanga)naomba kuuliza swali. Jumapili ile 'tukufu ya mapinduzi' ilitazamiwa washindi ama wawe Chelsea (99%)ama Manchester United (1%)ilikuwaje kombe lenyewe likawepo Stanford Bridge? Ingekuwaje kama ingetokea miujiza Manchester akabahatisha? Au kulikuwa na makombe mawili? Na kama ni hivyo, huwa inakuwaje ikiwa timu zaidi ya 2 (sema 4 za miji tofauti) zinatazamiwa kunyakua ubingwa? Kombe lilikuwa wapi kabla ya dakika ya mwisho?

Ninaamini katika ufanisi wa usafiri uingereza hasa wa treni na anga lakini kati ya London (waliko Chelsea)na Manchester ni zaidi ya Kilomita 263. Je kombe lilisafirishwa katika dakika chache baada ya mipira kumalizika kote. Natamani kujua nini kilitokea ama nini hutokea.

Labels: , ,

3 Comments:

At 4:44 AM, Blogger Fadhy Mtanga said...

Kaka una mbwembwe kweli. Hadi leo husahau tu? Najua umekusudia kutonesha vidonda vya watu. Mmebahatisha.

Hilo swali la kombe nami nilijiuliza sana siku ile. Kwa bahati mbaya nikauliza watu niliokuwa nao lakino hawakuwa na majibu.

Jumatatu nimejaribu kudadisi hilo jambo. Lakini majibu yanaonesha lilikuwa centralized somewhere ili iwe rahisi kwenda any direction. Na kwa akili ya kawaida (ya kuambiwa nikachanganya na yangu) kwa jinsi score ya Chelsea hadi halftime, ilitosha kabisa kufanya decision kombe lisogezwe wapi?

Hongereni sana ila punguzeni kelele maana mmebahatisha.

 
At 4:47 AM, Blogger Fadhy Mtanga said...

Nilisahau jambo. Nimegundua ubaguzi wa rangi bado upo katika EPL. Lampard aliona ni kheri mzungu mwenzake Rooney japo ni timu tofauti (huko Mbeya mnasema tafwauti) kuliko kuchukua ngozi nyeusi.

 
At 6:49 AM, Blogger John Mwaipopo said...

fadhy mtanga asante kwa ufafanuzi huu. nadhani unaingia akilini ukizingatia udogo (au ukubwa) wa nchi yenyewe na miundombinu kabambe hasa ya treni ya chini ya udongo.

nimeupenda huu msemo mpya aliouanzaisha raia namba moja wa 'akili za kuambiwa kuchanganya na zako'

 

Post a Comment

<< Home