MSAADA TUTANI

Wababe wa Ligi Kuu ya Uingereza wakijinafasi na kombe lao
Ikiwa ni juma la kusherehekea ushindi wa Chelsea wa Ligi Kuu ya Uingereza (najua huu sio wimbo mzuri kwa Chib na Fadhy Mtanga)naomba kuuliza swali. Jumapili ile 'tukufu ya mapinduzi' ilitazamiwa washindi ama wawe Chelsea (99%)ama Manchester United (1%)ilikuwaje kombe lenyewe likawepo Stanford Bridge? Ingekuwaje kama ingetokea miujiza Manchester akabahatisha? Au kulikuwa na makombe mawili? Na kama ni hivyo, huwa inakuwaje ikiwa timu zaidi ya 2 (sema 4 za miji tofauti) zinatazamiwa kunyakua ubingwa? Kombe lilikuwa wapi kabla ya dakika ya mwisho?
Ninaamini katika ufanisi wa usafiri uingereza hasa wa treni na anga lakini kati ya London (waliko Chelsea)na Manchester ni zaidi ya Kilomita 263. Je kombe lilisafirishwa katika dakika chache baada ya mipira kumalizika kote. Natamani kujua nini kilitokea ama nini hutokea.

