SAUTI YA BARAGUMU
WAAMINIFU WANAAMINI BARAGUMU LIKIPIGWA LINA JAMBO, TENA JAMBO JEMA. BASI BARAGUMU HILI LINAJITAHIDI KUFIKIRISHA, KUFUNZA NA KUBURUDISHA
Wednesday, December 17, 2008
Friday, December 05, 2008
Ndanda Kosovo ndani ya Nyumba Tena
Yule Mkongomani aliyetikisa sana anga za Tanzania kwa muziki wa dansi yenye mirindimo ya Ki-Kongo almaarufu Ndanda Kosovo ameibuka kivyengine. Yupo na bendi inaitwa Watoto wa Tembo International. Haya tusubiri nini katuandalia Krisimasi hii. Sie yetu macho na starehe tu wakongo wanaposhindana.
Labels: muziki
Monday, December 01, 2008
Chelewa Chelewa Harusini Stivini na mkewe (jina la shemeji wangu nimilisahau) wakimeremeta
Shida ya kuchelewa kwenye sherehe ni hii ya kupata kiti sehemu ambazo waliowahi huwa-ga hawazitaki ama wanazikwepa-ga. Juzi nilishiriki harusi moja. Ukikaa sehemu hii watu waendao huko woote lazima wapite kukusalimia ama kabla ya kuingia huko ama baada ya kutoka huko. Lakini mambo yetu yale kama kawaida.