Monday, December 01, 2008

Chelewa Chelewa Harusini Stivini na mkewe (jina la shemeji wangu nimilisahau) wakimeremeta



Shida ya kuchelewa kwenye sherehe ni hii ya kupata kiti sehemu ambazo waliowahi huwa-ga hawazitaki ama wanazikwepa-ga. Juzi nilishiriki harusi moja. Ukikaa sehemu hii watu waendao huko woote lazima wapite kukusalimia ama kabla ya kuingia huko ama baada ya kutoka huko. Lakini mambo yetu yale kama kawaida.

11 Comments:

At 7:22 AM, Blogger Christian Bwaya said...

Mwaipopo una mambo. Ha ha aha aha aaa! Du. Naweza pata picha ya hali ya hewa ya hapo ulipokuwa...!

Swali la msingi linaweza kuwa "...Kwa nini hukuona tabu kuitumia 'siti' hiyo ambayo kimsingi ingekimbiwa na wengine?"

Nilichojifunza: Ukitaka kumtambua mtu anavyojichukulia tazama anavyoweza kuyafanya maisha yawe rahisi. Nikiwa na maana namna asivyoruhusu mazingira kutawala namna anavyoonekana ama kuhisi watu wanamwelewaje katika mazingira husika kwa kumlinganisha na hadhi aliyonayo tayari.

Japo siwezi kuhitimisha kwa tukio hili moja tu, hata hivyo ninaweza kufanya bashiri ya haraka haraka kwamba wewe ni mtu uliyejikubali na huna shaka na namna ulivyo, wanavyokuchulia wengine na hata namna unavyoweza kuishi na wengine.

Inafurahisha kuona watu wanaojielewa wasihitaji kuhangaika na kumaintain P (Sore sina kiswahili chakeeee).

Samahani nimeandika sana mpaka nimesahau nilichotaka kusema. Kazi nzuri.

 
At 12:00 PM, Blogger Fadhy Mtanga said...

Kaka harusi bila shaka ilikuwa njema.
Labda nikuulize, hivi ni kwanini hasa watu huwa wanazikwepa siti hizo?

 
At 2:49 AM, Blogger John Mwaipopo said...

Bwaya nimefurahi kukuona hapa. Mbali na sura yenyewe sehemu yenyewe ilikuwa vema sana. Mosi ukiingia huko ndani unatokomea mbali kidogo na pia kulikuwa kusafi vya kutosha. pili kukaa hapo kulinifanya nisionekane kirahisi na wanyakyusa waliosafiri toka kyela. Walikuwa wanasikia tu kuwa nipo lakini hawanioni. Si unajua tena mazungumzo yangekuwa mengi kuliko shughuli iliyotupleka pale.

Mtanga shughuli ilikuwa supa sana. Hata mimi sijuagi kwa nini watu hupakwepa sehemu kama hapa. Pengine hofu yao ni mijiharufu itakapoanza, jambo ambalo kwangu halikutokea kwa sababu nilizozitoa pale juu.

 
At 5:42 AM, Blogger Egidio Ndabagoye said...

Ebwana dah! natumaini gari la huduma halikukauka maeneo yako.Harusi imependeza

 
At 5:42 AM, Blogger Egidio Ndabagoye said...

Ebwana dah! natumaini gari la huduma halikukauka maeneo yako.Harusi imependeza

 
At 11:44 PM, Blogger tosha said...

ebana harusi ilikuwa poa kchz namna..ila mwaipopo nakuaminia we mgumu huna ubitozi wakaa popote tu...mi tosha mezza mwanafunzi wako mwaka 2003 pale TIA Mby

 
At 5:32 AM, Blogger John Mwaipopo said...

Nimekusoma tosha ukwapi siku hizi. Nahisi untakuwa umefunika bovu. nakukumbuka sana. karibu

 
At 9:39 PM, Blogger tosha said...

niko dar kaka naish maeneo ya kijitonyama karibu na sayansi.
na kazini kwangu ni tume ya sayanzi niko jirani tu mzee.nimeoa mwaka jana mwishoni utanisamehe sikukupa taarifa .lkn namshukuru mungu tu wazima na tumeuona mwaka 2009

 
At 2:04 PM, Blogger paesulta said...

pole sana ndugu,i can imagine, kweli hiyo sit haijakaa sawa kabisa,lakini nina imani kuwa ulifurahia shughuli yenyewe ya harusi,kwani ndio kitu muhimu...
Mdau,
Thessaloniki,Ugiriki.....

 
At 10:35 PM, Blogger Othman Michuzi said...

hahaha ahahah ahahaa

hii imetulia sana mkuu,yaani nimecheka hadi basi na hayo mamneno yako mkuu.

pamoja kwa sana kaka.

 
At 1:33 PM, Blogger MICHUZI BLOG said...

Tehe tehe tehe tehe..... sasa hapo bufee unalia mezani ama unarudi na pleti yako papo hapo? aisee you made my day! mambo vp huko ticha, natia timu karibuni.

 

Post a Comment

<< Home