Saturday, June 23, 2007


Ni Katika Afrika tu !!

Ni katika Afrika tu ndiko kuna mwanafunzi wa shule ya msingi mzee kuliko wote duniani. Mzee huyu, Kimani Ng'ang'a Marunge (pichani) aliamua miaka mi-4 iliyopita kuwa elimu ni ufunguo wa maisha na kwa kuwa alikuwa hana basi aende shule kujifunza kusoma na kuandika. Ana miaka 87 sasa. Malengo yake ni kuwa daktari. Kama huyawahi kumsoma msome hapa na hapa. Heko sana mzee wangu, sidhani kama wazungu wanaweza kuchukua uamuzi kama huu au?

Friday, June 15, 2007

Karibuni Lanchi

Washikaji wote karibuni lanchi mchana huu. Hakika siwezi kumaliza baga lote hili. Ila cheese haipo ya kutosha na kwa mnaotumia Coke ipo ya kutosha. Ulanzi na komoni vipo. Mnaotumia vinywaji vingine mje navyo wenyewe. karibuni

Thursday, June 14, 2007

HAIFAI KUCHELEWA MIKUTANONI
Alexander Mwalyoyo wa Tanganyika Yetu kanitumia hii nami nawabandikia ambao hamjawahi kuiona.
A priest was being honoured at his retirement dinner after 25 years in the Parish. A leading local politician and member of the congregation was chosen to make the presentation and give a little speech at the dinner.
He was delayed, so the priest decided to say his own few words while they waited.
"I got my first impression of the parish from the first confession I heard here. I thought I had been assigned to a terrible place. The very first person to enter my confessional told me he had stolen a television set and, when questioned by the police, was able to lie his way out of it. He had stolen money from his parents, embezzled from his employer, had an affair with his boss' wife, taken illegal drugs and he had given VD to his sister.
"I was appalled. But as the days went on I knew that my people were not all like that and I had, indeed, come to a fine parish full of good and loving people."
Just as the priest finished his talk, the politician arrived full of apologies at being late. He immediately began to make the presentation and gave his talk. "I'll never forget the first day our parish priest arrived, said the politician. "In fact, I had the honour of being the first one to goto him in confession....."
Everybody burst into laughter
Moral of the story: DON'T BE LATE for meetings.

Tuesday, June 12, 2007

Usitake Ncheke Mie!!!! Kumbe kazi ya U-DJ sio ngumu. Katuni zingine za kutisha (kama unatumia pombe na sigara zinatisha ) za David Chikoko zibofye hapa.

Watoto wa shule Tanzania wakutwa na silaha za maangamizi
He kumbe ujambazi bongo waanzia shuleni. Hivi sisi ni kizazi cha namna gain. Lakini pengine sio Bongo tu. Bongo watu wakichapana kwa visu ughaibuni wachapana kwa risasi. Mtoto alelewavyo ndivyo atakavyokyuwa. Eti bongo watoto wakamatwa na silaha shuleni. Watoto wakora hawa. Ila sijui ni kweli au chumvi kibao. Je wakikuwa si watakuwa wameshazoea ukora ama utukutu. Ukishasoma kwa kubofya hapa niambie ama tafakuri mwenyewe tufanyeje.

Monday, June 11, 2007

Pool Tabe Singida
Wandugu salaam. Ama baada ya hizi salaam nakutakeni radhi kwa wale mliotembelea hapa na kunikosa. Kauvivu kidogo na mambo mengine vilinitorosha. Lakini nilikuwa napitia pitia baadhi ya blogu ikiwemo ya Michuzi, Makene, Ndesanjo, Jeff Msangi na kadhalika.

Nguvu yangu ya kublogu imehuishwa na ziara yangu mkoani Singapore juma lilipopita. Kijana mmoja (alikataa picha) amebuni kwa siku mbili tu pool table yake kama inavyoonekana pichani. Sheria na kanuni ni zilezile isipokuwa umbile. Goroli ndio mipira. Nilicheza naye akaninyuka mbili bila.

Tupo pamoja