Monday, June 11, 2007

Pool Tabe Singida
Wandugu salaam. Ama baada ya hizi salaam nakutakeni radhi kwa wale mliotembelea hapa na kunikosa. Kauvivu kidogo na mambo mengine vilinitorosha. Lakini nilikuwa napitia pitia baadhi ya blogu ikiwemo ya Michuzi, Makene, Ndesanjo, Jeff Msangi na kadhalika.

Nguvu yangu ya kublogu imehuishwa na ziara yangu mkoani Singapore juma lilipopita. Kijana mmoja (alikataa picha) amebuni kwa siku mbili tu pool table yake kama inavyoonekana pichani. Sheria na kanuni ni zilezile isipokuwa umbile. Goroli ndio mipira. Nilicheza naye akaninyuka mbili bila.

Tupo pamoja

3 Comments:

At 9:51 PM, Blogger Unknown said...

Mwanangu hizi Pool Table nimezikubali, Wabongo tunaweza...
Si Mchezo.
Dah!
Hapo utacheza Mgongomgongo bila kujijua...
Balaa..!

 
At 9:10 AM, Blogger Christian Bwaya said...

Hongera kufika Singa, nyumbani kwetu. Hilo poool linaweza kuwa kibandani kwetu mitunduruni.

 
At 11:07 AM, Blogger jossy kigwa said...

wote walianza hivyo.tutafika.

 

Post a Comment

<< Home