Saturday, June 23, 2007


Ni Katika Afrika tu !!

Ni katika Afrika tu ndiko kuna mwanafunzi wa shule ya msingi mzee kuliko wote duniani. Mzee huyu, Kimani Ng'ang'a Marunge (pichani) aliamua miaka mi-4 iliyopita kuwa elimu ni ufunguo wa maisha na kwa kuwa alikuwa hana basi aende shule kujifunza kusoma na kuandika. Ana miaka 87 sasa. Malengo yake ni kuwa daktari. Kama huyawahi kumsoma msome hapa na hapa. Heko sana mzee wangu, sidhani kama wazungu wanaweza kuchukua uamuzi kama huu au?

3 Comments:

At 7:32 AM, Blogger mloyi said...

Elim haina mwisho, na mwanzo wake haujulikani.
Usishangae sana!

 
At 11:03 AM, Blogger jossy kigwa said...

inatia moyo.namwombea awe bingwa wa mifupa kwani atasaidia ajali zimezidi kwetu

 
At 5:16 PM, Blogger SimbaMkali said...

sema kwa shule ya msingi. lakini kwa elimu ya juu wapo waliomzidi umri. kwa mfano hawa

http://www.nis.wvu.edu/Releases_Old/ocie.htm

http://www.usatoday.com/news/offbeat/2006-11-21-lifelong-learner_x.htm

kwa vyovyote vile, lazima tumpe sifa mzee wetu. hii iwe ni changamoto kwa watoto na vijana kujiendeleza kielimu. safi sana.

 

Post a Comment

<< Home