Monday, July 19, 2010

NIMEWAHI KUWA PWEZA

Awali ya yote nikusalimieni wote ambao mlikuja hapa lakini mkanikosa. Sababu za kutopatikana zilikuwa mbili. Mosi nilikuwa safarini ambako kulinibana hata kushindwa kupata internet. Hata nilipopata wasaa wa kuchungulia internet, sababu ya pili, mtandao haukuwepo.

Wakati wa mimi kutokuwepo hewani kombe la dunia liliendelea na kumalizika. Katika matukio yaliyonisikitisha kuhusu kombe la dunia la mwaka huu ni kutolewa 'timu yangu ya Brazil' katika hatua ya pili tu. Huwa nawapenda sana Brazil.Flagi la Brazil

Kabla ya Kombe la Dunia kuanza nilitoa angalizo na kukata tamaa kwangu kuhusu kufanya vema Brazil. Baada ya kusikia Brazil wanakuja kucheza na Taifa Stars niliogopa na kuandika sehemu fulani maneno haya chini.Kamba unabisha soma hapa, nenda maoni ya 11

kwa nia njema tu nawaomba brazil wasije kucheza na taifa stars. stars sio kipimo cha brazil. labda ni kipimio cha kupunguza ukali wa brazil.

pili stars imekuwa ikizipa nuksi timu zinazocheza nazo kwa maandalizi ya mashindano makubwa. walianza new zealand. walipoenda afrika kusini kwenye kombe la shirikisho wakawa urojo na kutolewa mapema.

wakafuata ivory coast. walipenda angola kwenye AFCON wakawa asusa, wakatolewa mapemaa.

sasa brazil ndio wanataka kuja kupata upako wa kufanya vibaya.

kwa mashindano ya world cup mwaka huu hali ya hewa ya dar es salaam haifai kwa training. Dar ni joto, Durban ni baridi. labda brazil waende njombe.


Baada ya Brazili kutolewa nikasikitika lakini nikawa nimetabiri kama pweza paulo alivyokuwa akitabiri vyema.

Labels: ,

2 Comments:

At 1:23 PM, Blogger Mija Shija Sayi said...

Mwaipopo umenichekesha leo. Yaani Stars imekuwa ni chanzo cha nuksi kwa timu zingine, ama kweli una jicho la ndani.

Ubarikiwe.

 
At 1:22 AM, Blogger poker said...

PROMO DELIMA
poker online | Agen Domino | Agen Poker|Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | bandar qiu | Judi online terpercaya

Bonus yang kami sediakan :
* TO (Turn over) sebesar 0.3% yang akan di kami bagikan setiap hari senin
* Bonus referal sebesar 10%

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat.
Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: Facebook
Phone number_: +85595678845

 

Post a Comment

<< Home